asas

asas

sintah

sintah

DR MENGI AZINDUA MPANGO WA AIRTEL FURSA TUNAKUWEZESHA JIJINI DAR


Dar es Salaam Mei, 27 2015: Airtel Tanzania imezindua programu mpya iitwayo Airtel Fursa itakayowawezesha vijana kiuchumi ikiwemo kuwapa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kupata maendeleo zaidi katika shughuli zao.

Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo, Mgeni wa heshima na  mfanyabiashara mkubwa nchini Dokta Reginald Mengi aliipongeza Airtel kwa kubuni program hiyo itakayosaidia vijana nchini huku akitoa wito kwa vijana wote nchini kuikumbatia fursa hiyo ili kuweza kutimiza malengo yao.

“Hii ni Fursa ambayo vijana wanatakiwa kuikumbatia kwa nguvu zote ili wale wote watakaofaidika waweze kuwashawishi wenzao pia katika miaka ijayo,” alisema”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema vijana watanufaika kwa njia mbalimbali na wataweza kujiendeleza kiuchumi na kupunguza suala la ukosefu wa ajira.

“Airtel FURSA itawawezesha vijana toka sehemu mbalimbali nchini, Fursa zitawafikia vijana wengi wenye kiu na ari ya kufanya ambacho wanakiamini na ambao wako tayari kukabili changamoto mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao na kubadilisha hali yao kimaisha,” alisema Colaso.

Alisema program hiyo inawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao.

Mbali na kutoa vifaa hivyo, Bw, Colaso alisema zaidi ya vijana wapatao 1500 watapata mafunzo mbalimbali ya kibiashara kila mwaka kupitia program hiyo.

“Watafundishwa kuhusu usimamizi bora wa fedha, namna ya kupata mikopo, namna ya kufugua akaunti benki na mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa biashara,” alisema Colaso.

Alisema program hiyo itahusisha vijana kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Mtwara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Airtel Balozi Juma Mwapachu, aliwataka vijana kutumia program hiyo ya Airtel Fursa kujiendeleza. Huku akiwaomba watanzania kuwapendekeza vijana wote wanaoona wanafaa kufaidika kwa mradi huo kwa manufaa ya jamii zao.

Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- JIna, Umri, aina ya biashara na eneo.

Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com.  ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, aina ya biashara na sababu ya kuomba msaada kutoka Airtel.

Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com.

“Programu hii itanufaisha vijana ambao tayari wana miradi mbalimbali na sio ambao wanataka kuanzisha,” alisema.

MWISHO

No comments:

Post a Comment