asas

asas

sintah

sintah

DR SLAA AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

1.Napenda  kumshukuru  mwenyezi  mungu  kwa  kutujalia  uzima.


2. Nimeamua  kujitokeza  leo  hii  ili  kukomesha  upotoshaji  na  kuuweka  wazi  ukweli.
3.Sina  tabia  ya  kuyumbishwa  na  ninasimamia  ninachokiamini.4.Sina  ugomvi  na  kiongozi  yeyote  maana  siasa  sio  uadui.5. Siasa  inapoongozwa  kwa  misingi  ya  upotoshaji, matokeo  yake  ni  vurugu.6. Naweka  wazi  kuwa  mimi  sikuwa  likizo  na  hakuna  mtu  yoyote  aliyenipa  likizo.7.Kilichotokea  ni  kuwa  niliamua  kuachana  na  siasa  tangu  tarehe  28.7.2015  saa  sita  usiku  baada  ya  kutoridhishwa  na  kilichokuwa  kinaendelea  ndani  ya  chama  changu.8.Ni  kweli  nilishiriki  kumleta  Lowassa  CHADEMA  Lakini  nilikuwa  na  misimamo  yangu  ambayo  ilitufanya  tusielewane. 


9. Baada  ya  Lowassa  kukatwa  pale  Dodoma, Gwajima  ambaye  ni  mshenga  wa  Lowassa  alinipigia  simu  kutaka  kujua  ninii  cha  kufanya.10. Nilimpigia   Mwenyekiti    Mbowe  kumjulisha  na  tukakubaliana  kupanga  muda  wa  kuwasikiliza.11. Kabla  ya  kuanza  kuwasikiliza, msimamo  wangu  ulikuwa  ni  kumtaka  Lowassa  kwanza  atangaze  kuhama  chama, aweke  wazi  ni  chama  gani  anaenda  na  ajisafishe  juu  ya  tuhuma  zake
12.Tangu  akatwe  jina, Lowassa  hakutangaza  kujitoa  CCM  na  wala  hakujisafisha  na  tuhuma  zake, kitu  kilichonifanya  nitofautiane  naye.
13. Niliwauliza  wanachadema  wenzangu  kuwa  Lowassa  anakuja  kama  Mtaji  au  Mzigo?
14. Swala  sio  urais  kama  watu  wanavyozusha, mimi  nilikuwa  nataka  mgombea  mwenye  uwezo  na  sifa  ambaye  ataweza  kuitoa  CCM.  Sikuwa  na  tamaa  ya  urais  kama  watu  wanavyosema 
15. Tangu  Gwajima  atupe  taarifa  za  ujio  wa  Lowassa, Swali  langu  la  Lowassa  kuwa  Mtaji  au  mzigo  halikuwahi  kujibiwa.
16. Nilitaka  kujua  ni  mtaji  gani  lowassa  atakuja  nao  na  ni  viongozi  gan  atakuja  nao.
17. Nilijibiwa  kuwa  anakuja  na  wabunge  50  wa  CCM, wenyeviti  22  wa  mikoa  na  wenyeviti  80  wa  wilaya.
18.Baada  ya  ahadi  hiyo, nilitaka  sasa  nipewe  majina  ya  hawa  watu  lakini  mpaka  tarehe  25  july  sikupewa  hayo  majina 
19. Wenzangu  waliniambia  kuwa  tarehe  27  niitishe  kikao  cha  dharura  ila  niligoma  kwa  sababu  nilikuwa  sijapewa  haya  majina 
20. Ndani  ya  kikao  hicho,  tulianza  kwa  mabishano  makali  kati  yangu  na  Mbowe, Lissu  na  Gwajima, viongozi  wenzangu  ni  shahidi  na  mungu  anajua. Msimamo  wangu  ulikuwa  ni  uleule  kujua  mchango  wa  Lowassa 
21. Kikao  kile  kikavunjika, baadae  tukaingia  kamati  kuu  lakini  bado  msimamo  wangu  ulikuwa  ni  uleule. Baadae  nikaandika  barua  ya  kujiuzulu.
22.Profesa  Safari  aliichana  ile  barua. 
23.Cha  kusikitisha  ni  kuwa  Kesho  yake  picha  zikaanza  kusambaa  mtandaoni  zikimuonyesha  na  lowassa  japo  viongozi  wangu  walizikana  zile  picha.  Kibaya  ni  kuwa  viongozi  waliuficha  ukweli 
24.  Kesho  yake  niliandika  tena  barua  rasmi  ya  kujiuzulu. 
25. Baada  ya  pale  zikaanza  propaganda  za  uongo  zikimuhusisha  hadi  mke  wangu  eti  kanizuia.
26. Naomba  watanzania  wajue  kuwa  mke  wangu  hakuwahi  kunizuia  kwa  lolote, lkn  hata  angefanya  hivyo  sio  mbaya  maana  hata  yeye  ni  mwanaharakati  mwenye  uchungu  na  nchi  hii. 
27. Mke  wangu  aliwahi  hadi  kuumia  wakati  akipigania  ukombozi  wa  nchi  hii.....Lakini  sio  mbaya, familia  yangu  imezoea  propaganda. 
28. Kikubwa  katika  harakati  ni  credibility  ambayo  lazima  uilinde  na  mimi  sitaki  jina  langu  liharibiwe  na  ni  haki  yangu.
29. Maslah  mapana  ya  taifa  ndiyo  yaliyotufikisha  hapa  na  sio  maslahi  binafsi. 
30.Lowassa  na  wapambe  wake  ni  waongo  maana  hakuna  hata  kipengele  kimoja  walichokitekeleza.
31. Tulitaka  hao  wabunge  50  waje  kwanza  kabla  ya  mchakato  wa  uteuzi  ccm
32. Napinga  kuchukua  makapi  ya  CCM  na  kuyaita  MTAJI.
33.Mtu  kama  Sumaye  ni  FISADI  na  nilikuwa  siongei  naye 
34. Sumaye  aliwahi  kusema  CCM  wakimchagua  Lowassa  atahama  chama. Leo  Lowassa  kawaje  msafi?? 
35. Tulitaka  Mtaji  toka  kwa  Lowassa  na  sio  MAKAPI 
36. Wenyeviti  walioletwa  na  Lowassa  ni  MIZIGO  na  namjua  vizuri. Akithubutu  kunijibu  ntamwaga  UOZO  wake  wote 
37.Nani  asiyejua  Guninita  pia  ni  mzigo??
38:  Nawataka  viongozi  wangu  wanijibu  ni  mtaji  upi  walioupata  toka  kwa  Lowassa.
39. Mimi  ni  Padri  Mstaafu, sipendi  siasa  za  uongo. 
39. Ukisema  unataka  kuiondoa  CCM  ni  lazima  ujikumbushe  misingi  ya  CHADEMA  ambayo  ilikuwa  ni  uadilifu. Leo  chadema  hii  ina  Uadilifu  gani?? 
40.  Namshangaa  sana  Lowassa  eti  kusimama  mbele  ya  watu  akijinasibu  kuwa  ni  msafi.....kwamba  mwenye  ushahidi  aende  Mahakamani. Ni  dhambi  kupotosha  watu.
41. CCM    hawana  ujasiri, ni  waoga  na  ndiyo  maana  wamewalea  watu  kama  akina  Lowassa 
42. Ukitoa  kinyesi  chooni  na  kukipeleka  Chumbani  maana  yake  hata  chumba  chako  ni  CHOO  na  kitakuwa  kinanuka  zaidi  kuliko  choo  cha  kawaida 
43.Mimi  nilikuwepo  wakati  sakata  la  Richmond  likijadiliwa.Mimi  nina  ugomvi  wa  muda  mrefu  na  Lowassa.
44.  Mwaka  2010  mimi  nilimtaka  Lowassa  atangaze  Richmond  ni  ya  nani.
45. Leo  tena  namtaka  Lowassa   Lowassa  atoke  hadharani  atangaze  Richmond  ni  ya  nani.  Unaposema  ni  ya  mkubwa, atuambie  mkubwa  gani
46. Ukitaka  kuijua  Richmond  rejea  Ripoti  ya  Mwakyembe. Nampongeza  Mwakyembe  na  Sitta  kujitokeza  hadharan  kuusema  ukweli.
47. Siku  moja  kabla  ya  ripoti  kusomwa, nililetewa  Rushwa  ya  milioni  500  ili  tukaupindishe  ukweli  bungeni  lakini  nilikataa 
48. Ripoti  ya  mwakyembe  iliamua   mambo  mawili,  moja; Lowassa  ajipime  au  bunge  lijadili  na  lichukue  hatua.  Lowassa  kuona  hivyo  akaamua  kukimbilia  kujiuzulu  kukwepa  aibu  ya  kung'olewa  na  bunge 
49:  Lowassa  haaminiki, ni  muongo  na  hastahili  kuwa  Rais  wa  nchi....
50.  Lowassa  ni  FISADI  na  kama  mimi  ni  muongo  ajitokeze  hadharani  akanushe
51. Anasema  Lowassa  ataleta  maji, mbona  jimbo  lake  la  Monduli  halina  Maji???
52.  Mnasema  Lowassa  kaanzisha  shule  za  kata, iv  mjua  msingi  wa  shule  za  kata?  waandishi  rudini  shule  mkajifunze  upya.
53.Nilifanikiwa  kuijenga  Chadema  na  ikawa  tumaini  jipya  la  watanzania.....Vijana  wangu  wa  Chadema, naomba  niwe  mkweli  propaganda  imekivamia  chama.
54.  Inasikitisha  kuona  CHADEMA  inajazwa kwa mabasi  pale  jangwani .....alafu  mnawadanganya  watu  eti  ni   MAFURIKO
55.  CHADEMA  ya  kipindi  changu  ilikuwa  inakemea  Rushwa. Niambien  leo  chadema  watasema  nini  kwenye  majukwaa? 
56. Mnaomtetea  Lowassa  na  nyie  jitokezen  hadharani...mimi  nasema  kwa  sababu  nina  ushahidi  na  sio  lazima  ushahidi  huu  niupeleke  mahakamani.
57. Wenye  uwezo  wa  kumpeleka  Lowassa  Mahakamani  ni  Serikali, na  mwakyembe  alisema  juzi  kuwa  kesi  ya  jinai  haina  kikomo, mtu  anaweza  kushitakiwa  muda  wowote 
58. Sitaki  kuingila  swala  la  Babu  Seya, lakini  waliolawitiwa  ni  watoto  waliokuwa  chini  ya  umri. kwa  nini  haki  yao  ipotee?
59.  Rais  hana  mamlaka  ya  kumtoa  Babu  Seya. Lowassa  asiwadanganye.
60.  Kuhusu  swala  la  Masheikh, Sumaye  ndiye  aliyeamuru  mapolisi  wavamie  misikiti  wakiwa  na  mbwa......Watanzania  msikubali  kudanganywa. hizo  ni  propaganda  za  wasaka  urais 
61. Masikubali  Rais  Muongo  na  mimi  naapa  ntapiga  kelele  kila  kona  kumpinga  Lowassa.
62.Lowassa  alipokuwa  waziri  mkuu, matatizo  yanayotokea  leo  hayakuwepo?  mapigano  ya  wakulima  na  wafugaji  hayakuwepo?
63.  Lowassa  akiwa  waziri  mkuu  alisababisha  migogoro  mizito  sana  kati  ya  monduli  na  karatu.  Rais  wa  aina  hii  wa  nini?
64.  Naomba  nisiongee  mengi  kwa  sababu  ntakosa  ya  kusema  siku  nyingine.....Nawataka  Lowassa  na  Sumaye  wajitokeze  kunijibu.
65. Siku  nyingine  ntakuja  kuongelea  kuhusu  hisa  za  Lowassa  kwenye  makampuni 
66.  Nahitimisha  kwa  kusema  kuwa  Nimestaafu  siasa  na  sina  chama  lakini  nina  nchi, hivyo  ntaendelea  kuwatumikia  watanzania  kwa  jinsi  mungu  alivyonipa  vipawa 

67.  Narudia  tena, Sina  chama  na  sitajiunga  na  chama  chochote. 
Waandishi  wanauliza  Maswali:  Mwandishi:  Umesema  hujiungi  na  chama  chochote, utawasaidiaje  watanzania?  Rais  gani  unamuunga  mkono?
Mwandishi  Guardian:  Ulisema  Lowassa  atakuwa  assert  kama  atakuja  na  wabunge  na  hao  wenyeviti.  Je  angekuja  kama  assert  ungeyasema  haya  yote?
Mwandishi  binafsi:  Umesema  waliohamia  Chadema  ni  makapi.  Mwaka  1995  Uliihama  CCM,   ukahamia  chadema. Je  na  wewe  ni  KAPI?
Mwandishi-Azam:  Umetangaza  kustaafu  siasa, lakini  bado  unakadi  ya  CCM  na  CHADEMA?  Je  utazirudisha?
Mwandishi  Blog:  Inaonekana  baada  ya  chedema  kukutosa  ndo  maana  unamshambulia  Lowassa, je  ni  kweli?
Majibu: 1. Kadi  ni  mali  zangu  na  siwezi  kuzirudisha. Ya  chadema  nimeilipia  miaka  20,ya  CCM  bado  haijaisha  muda  wake.
2. Kuhusu  urais, mimi  sijagombea  urais  na  sikuchukua  fomu.  sasa  kwa  nini  nikasirike  kisa  wamempa  Lowassa? Sina  ugomvi  na  Mbowe  na  nakumbuka  alinisaidia  nyumba
3.  Mimi  sio  KAPI....Ili  kuujua  ukweli  unahitaji  kutumia  kigezo. KAPI  ni  yule  aliyekataliwa  na  chama  flani, mimi  sikuwahi  kukataliwa.  Sikuwa  na  uchafu  wowote  wakati  naingia  CCM.
4.  Lowassa  ni  mzigo  tu  hata  kama  angetuletea  hao  watu  wake.....Lowassa  ana  makandokando  mengi. Angetuletea  hao  watu  ndo  tungeamua  tumpokee  au  tusimpokee
5.Mimi  sina  chama  na  sitampigia  kampeni  mtu  yeyote. Mimi  nimefanya  utafiti  kwa Lowassa  pekee, kwamba  taifa  litapata  madhara  gan  Lowassa  akiwa  Rais.....Lowassa  ni  Fisadi.
 
 -Kazi  yangu  leo  ilikuwa  ni  kuwaambia  watanzania  waachanane  na  ushabiki.Ukihamishia  CHOO  chumbani, manake  harufu  itahamia  huko.
 -Chadema  ya  leo  kwa  sasa  imetekwa  na  Lowassa  na  hawawezi  tena  kuongelea  Ufisadi 

Maswali  ya  nyongeza
1.Umesema  waliohamia  chadema  kwa  sasa  ni  sawa  na  mfano  wa  Choo. Je, wewe  ulipohama  hukuwa  choo?  kwa  nini  wewe  uliweza  kukibadili  chama  halafu  akina  Lowassa  washindwe?
Jibu:  Wakati  mimi  nahama  sikuwa  mchafu  kama  hawa  akina  Lowassa  na  Sumaye.

49 comments:

 1. nilisikiza jana na nimefurahi kuiona tena hii speech hapa tena kwakweli tuchozi zinanitoka ilikuwa superb kweli chadema wamepoteza lulu kwa kurukia makapi sielewi upinzani unaenda wapi,,, its so funny wandishi hawakuwa na masuali ya msingi ata moja yani unaona vile wameegemea upande mmoja kweli sekta ya habari imekufa tz aisee!! mfano uyo alieuliza kama dk slaa alipohama ccm kwenda chadema lol are u for really??? tunazungumzia viongozi walihama chama baada ya kuchugwa si ndio MAKAPI jameni msxiiiiiuu
  ??

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mmmh mdau umesema ukweli, Mi yale maswali ya waandishi tu hoi!!

   Delete
 2. Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpa uhai Dr. Slaaa kwani watanzania walikuwa wanaangamia kwa kukosa maarifa. Kitu alichoongea Dr, Slaa ni muhimu sana kwa taifa letu. Jamani tuangalie sana maamuzi yetu tarehe 25. Tusije tukajuta hiyo miaka 5 ijayo na kuanza kuikimbia nchi yetu yenye neema na kukimbilia nchi za watu kwa shida tutakazozipata. Kwa ufupi UKAWA wamekuwa wasanii na sio upinzani tena. Mungu Mbariki Dr. Slaaa , Mungu ibariki TANZANIA. Amen

  ReplyDelete
 3. Honestly,umezidi kumuandama January makamba zote hizo ni personal conflicts zako unaziingiza kwenye reputation ya mtu..huoni ni wewe peke yako ndo umekomaa na hiyo allegations ya makamba ndio anahusika na shut up law! yani wewe tu ndio unajua kwamba anahusika huoni kama hizo ni allegations zisizo na msingi..au wewe ndio usalama wa taifa katibu..Honestly tumekuchokaaaaaaaa ujuaji mwingi kumbe huna unalolijua unapoteza tu energy kuandikaaa sometimes yasiyo hata na msingi...hivi hata unapata muda wa kukaa na Keanu wako...no wonder mashoga zako wanasema desparate house wife Buhahahaaaaa..kelele nyingiiiii sas si uwe unaenda mahala HUSIKA HATUA ZICHUKULIWE kama wewe mwanaharakati kweli..unaishia tu kupiga kelele tu kelele tuuu hatua zozote hatuzioni unazidi tu kuchanganyikiwa day by day...wewe ni January tu January tu au kisa mwammy ameswear to marry Naki jinsi anavyomkubali frendo wake ndio hasira unamalizia kwa kaka wa watu....msonyooooooo kafie huko sijui los angels sijui Atlanta maana bibvi wewe

  Mtaa wa pili

  ReplyDelete
  Replies
  1. Tumekuchokaa, we we na Nani? Andika kwa nafsi

   Delete
  2. Kachambie ganda la ndizi huku sio mahali pake.

   Delete
  3. kwani haya ugeyasema kwenya blog yake ugepugukiwa nini na why unaingia kwenye blog yake huyo ndo mange bwana utamfuata tu

   Delete
  4. Ukimwambia ukweli anabania comment. Kazibania zangu nyingi tu.
   Aache kua desperate sijui stress zimezidi. Yani anaandika vitu havina maana kabisa.
   Uwiii kalale mbele huko mwambie lance akutafutie kazi.
   Eti unapost vitu vya ukabila mara mgombea uraisi flani hii ndo nyumba ndogo yake. Hizo habari unazopewa changanya na akili yako sio kukurupuka tu ww low life desperate housewife.

   Delete
  5. SLAA NI KIBARAKA WA CCM...HANA TOFAUTI NA LIPUMBA.. MOTO WA WATANZANIA WA KUTAKA CCM IONDOKE MADARAKANI NI ULE ULE HATUYUMBISHWI NA VIBARAKA NJAA

   Delete
 4. Asante Sintah maana winging bundle ni shigda hii naweza printi hata nikasambaza. That shameless man. Alitakiwa atubu asubiri kupumzika kwa amani. Na sio kuendelea kusema uongo akifikiri atashinda huu uraisi Lowassa hatakaa awe raisi wa nchi hii period

  ReplyDelete
  Replies
  1. Shindwa wewe...Who are you hadi useme hawez kuwa rais! wait 25 oct you will see the wonders of Tanzanian!!!

   Delete
 5. Slaa umetumwa!! umelipwa kiasi gani?? Povu limekutoka huna haya hujui vibaya!! kama umestaafu siasa ungefunga bakuli lako kuliko hicho ulichokifanya!! kwa taarifa yako umechelewa pole sana!! ni bora ungeendelea kukaa kimya yaan M4C kama kawaaaaaaaaaaaaa piiiiiiiiiiiiiiipooooooooooooooooo

  ReplyDelete
  Replies
  1. Majib Ya lofa, si ujibu

   Delete
  2. kikatio si unacho fanya yako siku hiyo slaa muache kama alivyo ni haki yake ya msingi na huu ndo wakati wake muafaka wa kusema namengine kayatunza semeni su kina lisu aje

   Delete
  3. Yaani yeye mwenyewe ameshajionea kwamba its too late, hana la kutuambia huyu chadema mbele kwa mbele

   Delete
 6. Kwahiyo katika huo utafiti wako umewaona Lowasa na Sumaye? huna lolote wewe babu unatumiwa na CCM. uchu wa madaraka ndio unaokusumbua!! kama nafasi ulishapewa ulichemka acha na wenzio wajaribu. Rudi kanisani ukatubu ili ufanya kazi ya Mungu siasa itakutoa roho.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Dr. Slaa kafulia tu, akaona bora atumike tu na CCM

   Delete
 7. Bravooooooooo DR. SLAA kwa kuuammbia ukweli umma wa watanzania hasa vijana wanaopenda kufuata mkumbo. LOWASA hatufai kuwa RAIS wetu jamani. Kura zote kwa Magufuli. MAGUFULI OYEEEEEEEEEEEEE

  ReplyDelete
 8. Ukawa mna jazba matusi mnapanick mno. Mjibuni kwa hoja sio matusi

  ReplyDelete
 9. Nilijua tu nikiingia huku leo lazima nikutane na hii habari!! yaan wewe Sintah ni bendera fata upepo. Yaani nimegundua uandishi wako ni wakibaguzi, habari unazowekaga huku ni kama ifuatavyo:-
  1. Habari za kuiponda Ukawa.
  2. Habari za kuisifia CCM.
  3. Habari za kuwachamba usiowapenda
  4. Habari za kuwasifia unaowapenda.
  Acha ubaguzi hata kama wewe ni team Magufuli au una vi_team ushuzi vyako huko uchochoroni sisi havituhusu!! hizo zote ni habari!! na sisi wapenzi wa brog yako tunatofautiana kimtazamo, Huo ndio ushauri wangu hutaki funga kiblog chako maana kimekaa kinafki nafki.

  ReplyDelete
  Replies
  1. well said...kasinta ndo maana hakaolew kajinga sana#Lowasa Rais kwa taarifa yako

   Delete
 10. Slaa ulikuwa wapi kutangaza kustaafu siasa? umesubili hadi ukatwe ndio utangaze kustaafu? tunakujua wewe ni kibaraka wa ccm hilo halina ubishi Marimao yanakuhusu huna jipya Piiiiiiiiiiipoooooooooooooooo

  ReplyDelete
  Replies
  1. Lowasa alikuwa wapi kuhamia Chadema mpaka alipokatwa huko CCM.

   Delete
 11. slaa hana jipya kaona hajapewa nafac ya kugombea urais tu.hapa ni piiiiiiiiiiiiiiipoooooooooooooooo.

  ReplyDelete
 12. Mapenzi yakizidi saaaaaaaaana uwezo wa kutafakari hupungua.

  ReplyDelete
 13. Mapenzi yakizidi saaaaaaaaana uwezo wa kutafakari hupungua.

  ReplyDelete
 14. Yaani kazi niliyonayo hapa mtaani na kazini ya kuwapigia watu wavote ccm utafikiria nalipwa... hahhaha nakaa nao chini, nawapa darasa, natoa maovu yote ya ukawa watu wanasarender... CCM oyeee.. Magufuli Rais wangu.. 2015

  ReplyDelete
 15. Slaa bana, anasema aliletewa mil500 eti akaikataa, najiuliza kwanini asingeenda kushtaki takukuru kama kweli yeye ni mzalendo kama anavyodai na anahofu ya Mungu? pili anasema walikubaliana lowasa angeenda na wanachama 62 cjui wabunge cjui madiwani, najaribu kujiuliza kwaiyo angekuja nao kweli asingeondoka na kuongea aliyoongea?? najaribu tu kuwaza kwa sauti. nachukia siasa maana hawa wanasiasa wanacheza sana na akili zetu.

  ReplyDelete
 16. Mzee angetumia bsaraa za uzee angekuwa na heshima popote alipo heshima yake ipo sawa ila mchezo huo amechelewa tena saana,

  ReplyDelete
 17. piiiiiiiiiiiiiiipoooooooooooooooos.......Pessssssssssssaaaaaaaaaa Mbele

  ReplyDelete
 18. Huyu babu tuachane naye hatusaidii chochote, kama kumponda EL ameshapondwa saana, na kama anamuona ni choo mbona kamati kuu ya ccm walisema kwa midomo yao kuwa wanaimani na loawassa na katika mikoa yote aliyoenda kuomba kura lowassa ndio alipata kura nyingi za wadhamini wa ccm sasa iweje leo huyu babu amponde!!? aache uongo ni dhambi. Na kama alilijua hilo ni nini kilimfanya ashiriki katika mchakato wa kumleta Lowasa cdm!! atuache wana mageuzi na Lowassa wetu, tumeamua.
  mbona hata ccm kuna ufisadi wa kutisha na ndicho kinachotuchosha watz. Au alitaka tuchague ACT! maana hata hicho nacho muasisi wake alitimuliwa chadema kwa undumilakuwili wake! na hata huyu Dr. slaa naye ameonyesha undumilakuwili anasema EL ametoka ccm kwa kukatwa baada ya kushindwa jina lake kupita ukawa wamempokea, kwani yeye alitokea wapi na kwa sababu gani si ni hiyo hiyo ya kukatwa au!!! Mimi naona sisi watz ndio waamuzi ni nani tutakaempa nchi tarehe 25/Oct na siyo propaganda za kisiasa. watanzania tutafakari kwa makini na siyo kuanza kumuhukumu mtu eti kwa sababu slaa kaongea!! that is ney ney papa geee....

  ReplyDelete
  Replies
  1. Chukua soda baridi kwa mangi, ntakuja kulipa...Lowasa For President

   Delete
 19. hamana anayefata mkumbo kila mtu anajielewa na anamaamuzi yaka, hata akichagua kichaa ndiio aliomuona anamfaa

  ReplyDelete
 20. Wasanii ni CCM waliokaa madarakani zaidi ya miaka 20 hawana walichowafanyia wananchi wao, kila siku na hadithi zao za paukwa pakawa, watu wamechoka ndio maana wameona afadhali wachague mwizi kuliko kuichagua ccm

  ReplyDelete
 21. Vijana wakiamua wameamua hawarudi nyuma ni bora wamchague fisadi mmoja ndani ya chadema kuliko kuchagua mafisadi 100 ndani ya ccm,

  ReplyDelete
  Replies
  1. Habari ndio hiyo!! Nashangaa wamemuona Lowasa? mbona CCM ina mafisadi wengi sana!! na wengine wamepita kura za maoni majimboni kwao kama wakina Anna Tibaijuka na wengine kibao!! kwani hatuwajui? na sisi Ukawa tunamtaka huyo huyo mnayemnyooshea kidole!! tunajua kuna kitu nyuma ya PAZIA!! haiwezekani CCM jasho la kwapa linawatoka kwa ajili ya mtu mmoja tu Lowasa kunanini hapo????????? Tunajua nyota yake inang'aa ndio maana anawanyima USINGIZI hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Piiiiiiiiiiiiiiiiipoooooooooooooooozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz

   Delete
 22. lowasa baba yetu hata wakupake matope sisi tutakusafisha,ikiyakosa mabadiliko ndani ya ccm utayapata nje ya ccm

  ReplyDelete
 23. Lowasa mabadiliko, nabadiliko lowasa, wauwe tu kwa bresha baba

  ReplyDelete
 24. Sisi tunamtaka huyohuyo fisadi

  ReplyDelete
 25. Ukikiona cha nini mwenzako anasema atakipata lini, people power

  ReplyDelete
 26. Km gwajima alikuwa mshenga muolewaji ninani?

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hahahahaaaaaaaaaa umenifurahishaje mdau!! hapo muolewaji ni Dr. Slaa cjui mahali yake kalipwa kiasi gani na CCM. Ila atambue kaolewa pekeake sisi katuacha kama tulivyo!! sisi WAPUMBAVU na MALOFA tumeaka hatudanganyiki ng'ooooooooo

   Delete
 27. Fisadi ndo mzuri....huyo huyo ndo rais wang

  ReplyDelete
 28. Ukiweka ccm na matonya nitachagua matonya, nishasema

  ReplyDelete
 29. Nitamchagua lowasa na ukawa,jeuri mwenzie kusudi,wanazarau wananchi wahali yachini ccm,halafu huwamtu anaeongeakwanhuvu nakupayuka mpaka mshipawashingo unamsimama huwasimuelewi nasitaki kumsikiliza,bora chadema mlivyoamua kuachana na slaa,Alikuwa hanamvuto anaongea kwajazba mishipa ya shingo inamsimama kwakweli nilikuwa simfurahii,nanimefurahi alivyoondoka chadema namienimeingia rasmi ukawa kura ni huko.wengine hatupendikelele Au kutumianguvu nyingi tunataka akili nautashi wamtu,kelele za siasa zinachosha nawakiingia madarakani wanajisahau najeuri,kwavilesipendikelele nampa asiepigakelele lowassa nimemuelewa tokawaanze nae mpaka wamkate yehatukani walahajibishani namtu anafanyayake siokilamtu anapendakelele wengine tunapenda vitendo.

  ReplyDelete
 30. Haya mambo ndio huwa nayakataa mimi, haya nyie endeleeni kugombana sie tunaichagua Chama Kubwa CCM, Kila siku Malumbano sasa tukiwapa Nchi itakuwaje nendeni Mkajipange kwanza hapa hamna chenu kabisa, Yaani nusu nianze kuwaamini kumbe hamna lolote Asante Dr. Slaa kuniondoa kwenye mtego huu, Watu kugombana hakuishi kila wakati, nani anataka Viongozi wababaishaji just like U, Hebu fikiri ndio umewapa nchi kesho utasikia tu Wanapigana marungu Ikulu hawa. Si mlikubaliana nyie sasa imekuwaje yaani nyie IKULU NI 20100 Mkikua sio sasa.

  ReplyDelete
 31. Kama imepangwa imepangwa tuu.ila ni lazima wengi wapewe Haki zao..kusema kweli lowasa ana watu wengi hata achafuliwe vipi bado ni raisi

  ReplyDelete
 32. Haki gani si mpaka Mshinde sasa!! Shikamoo CCM!

  ReplyDelete
 33. Wanasema eti Lowasa mwizi mara oooh fisadi, mi nauliza hivi kwani tangu amestaafu kuwa waziri ccm hawajaiba tena? na kama wameiba hao wezi wapo chama gani kama sio ccm? We Magufuri tumeishakutaftia funguo na ufunguo wa kweli ni Lowasa hapo lazima ufunguke tuu utake usitake.

  ReplyDelete