asas

asas

sintah

sintah

ROSTAM ACHARUKAAA

Rostam Aziz

Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, amemvaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akimuita kuwa ni mtu mwongo, mbinafsi na mpotoshaji mkubwa.

Rostam alieleza hayo katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake jijini Dar es Salaam juzi, alipozungumza na vyombo vya habari kuelezea mambo kadhaa zikiwamo sababu za kujiondoa ndani ya Chadema.

Dk. Slaa alidai kuwa mwaka 2009 baada ya kutaja orodha ya mafisadi 11 nchini katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam,  Rostam alimpigia simu na kumtishia maisha.

Dk. Slaa pia alidai juzi katika mkutano wake na vyombo vya habari uliorushwa na vituo vitatu vya runinga kuwa Rostam anaifadhili Chadema.

Katika taarifa yake jana, Rostam alisema: “Nilimsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa jana (juzi) alipokuwa akizungumza katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

“Kwa mara nyingine kama ilivyo hulka yake miaka yote, Dk. Slaa kathibitisha pasipo na shaka kwamba yeye ni mbinafsi na mpotoshaji mkubwa.”

“Nimesikitishwa na kushtushwa japo sikushangazwa hata kidogo na hatua ya Slaa ambaye sasa anaonekana kukubuhu kwa uzushi kutoa matamshi ya namna hiyo.

"Sijapata hata mara moja kuwa na mawasiliano na Dk Slaa wakati wowote. Madai yake kwamba eti nilimtisha ni ya kupuuzwa na yasiyo na msingi hata kidogo,” alisema Rostam.

Rostam alieleza kuwa ni jambo lisiloingia akilini hata kidogo kwa watu wanaomfahamu Slaa kwamba anaweza kumtishia maisha na yeye akakaa kimya bila  kuchukua hatua ya kwenda polisi na kumshitaki halafu anakaa na jambo hilo kwa miaka yote hadi juzi ndipo alisema hadharani.

“Ili kuthibitisha madai yake hayo, namtaka Dk. Slaa kujitokeza hadharani na kutoa ushahidi wa jambo hilo,” alisema Rostam.

Huu ni uongo mwingine wa dhahiri. Namtaka Dk. Slaa kutoa ushahidi pia katika madai yake haya.
 
“Ni huyu huyu Dk. Slaa ambaye mwaka 2010 alizusha kwamba eti mimi, tukiwa na Rais Jakaya Kikwete na Edward Lowassa tulikutana katika hoteli ya La Kairo, Mwanza na kupanga njama za kumuibia kura zake za urais,” alisema na kuongeza:

“Wakati Slaa akitoa madai hayo ya uongo, mimi nilithibitisha kwamba wakati huo nilikuwa Afrika Kusini na Rais Kikwete akiwa Lindi huku Lowassa akiwa Arusha. Ni wazi kwamba tusingeweza kukutana La Kairo kama alivyodai yeye.”

Kwa mujibu wa Rostam, Dk. Slaa kuna wakati alimzushia hadi Rais Kikwete alipodai kwamba alisafiri kwa usiku mmoja kwenda China kumtoa mwanaye aliyekuwa amekamatwa na vyombo vya usalama, kisha kurejea Dar es Salaam usiku huo.

“Ni Slaa huyu huyu ambaye mwaka 2010 wakati wa kampeni alifikia hatua ya kuutangazia umma wa Watanzania kwamba kulikuwa na malori yaliyobeba kura za CCM ambazo zingesaidia ushindi wa wizi yaliyokamatwa Tunduma. Malori hayo yalipokaguliwa yalibainika kuwa na mizigo ya kawaida,” aliongeza katika taarifa hiyo.

21 comments:

 1. Slaa anatafuta kiki na sisi wananchi hatudanganyiki!! katapika pumba zake, kalamba mshiko then kasepa!! kifupi kajishushia heshima mwenyewe, uwezo wa kuisambaratisha UKAWA kwa sasa hana, labda kawapata wajinga wasiojitambua!! lakini mwenye akili timamu na anayesoma alama za nyakati hawezi kuyumbishwa na matapishi ya Slaa!! akiweza aje na mbinu nyingine maana Kodi za wananchi zipo na hayo ndio matumizi yake WELL DONE CCM. Ila mtambue safari yenu ya kifo iko mbele Oct, 25. 2015. Piiiiiiiiiipoooooooooozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz

  ReplyDelete
 2. CCM OYEEEEEEE!!!!!!!!!... UKAWA

  W A N A T E T E M E K A!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 3. power! ukawa oyeeeeeeeeeh! Lowasa!

  ReplyDelete
 4. Rostam na wewe sasa ni muongo.. Unakataa nini kuwa kikwete hakusafiri usiku kwa usiku kwenda kumtoa mwanae china alipokamatwa na madawa ya kulevya.. Hadi sasa kila mkataba wa uwekezaji wanapewa china kwa ajili ya kulipa uungwana aliofanyiwa kikwete wa kutolewa mwanane bila kuandikwa popote au kunyongwa... Unakataa kitu ambacho kipo wazi kabisa... Shame on u Rostam

  ReplyDelete
 5. huyo Rostam ni raia wa wapi mbona kama simsomi hivi???? I MISS IDD AMIN DADA....BIG UP SLAA wee ndo bullet ya mwisho walio baki wote matonyonyo

  ReplyDelete
 6. Huyu mzee ni noma anaongea uongo juu ya watu halafu tena anatumika tena kuongea uongo mwingine ni hatari sana.

  ReplyDelete
 7. Huyu mzee ni majanga alijua atawakomo ukawa kumbe kajikomoa mwenyewe, sasa anatapatapa tu hakuna wakudanganyikwa na ccm hata mje na sere ya kumwanga hela mitaani hatuwataki tumewachoka,

  ReplyDelete
 8. Slaa ulizani unabomoa kumbe ndio kwanza unazidi kujenga umetuongezeea umaarufu mara dufu,

  ReplyDelete
 9. mabadiliko.......... lowasa.......lowasa mabadiliko

  ReplyDelete
 10. Popote ulipo lowasa tutakufata wache wakuchafue tutakusafisha wenyewe kwa mikono yetu

  ReplyDelete
 11. Jihukumu mwenyewe Slaa kabla hujamuhukumu lowasa hakuna msafi hapa duniani

  ReplyDelete
 12. mchungaji gani anaishi kimada na mwanamke,

  ReplyDelete
 13. Slaa umekurupuka hata kama ulitumwa ungefikiri kwanza kabla ya kuongea

  ReplyDelete
 14. Embu aende kwao asia hukooo

  ReplyDelete
 15. Embu aende kwao asia hukooo

  ReplyDelete
  Replies
  1. KWAO THAILAND ANAKUJA KUTUFANYIA FUJO SIE , USO WAKE KAMA KOBE MZEE

   Delete
 16. CCM mnachekesha sana!! hamchoki kumchafua Lowasa?
  1. Mara Lowasa hafai ni fisadi
  2. Mara Lowasa hafai ni mzee
  3. Mara Lowasa hafai ni mgonjwa
  Na mimi nawauliza:-
  1. Hivi ndani ya CCM kuna mafisafi wangapi?
  2. Kati ya wanachama wa CCM 38 waliokidhi vigezo Lowasa hakuwepo??
  3. Kama Lowasa hakidhi vigezo au hana sifa kwanini Nec walitoa form kwa Lowasa kugombea Urais?
  4. Kama ni mgonjwa basi wangesema Rais wa Nchi achaguliwe na madaktari! kwanini anachaguliwa na wananchi?
  5. Nani mwenye uhakika wa kuishi milele hapa duniani??
  6. Nini maana ya kuunda Baraza la Mawaziri?
  7. Kwani Ikulu wanaenda kulima?? wengine waweze wana nini? hata yeye ashindwe ana nini??
  Endeleeni kumchafua mnapoteza muda!! Yaan sisi tunasonga mbele M4C kama kawa Piiiiiiiiiiipooooooooooooozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz

  ReplyDelete
  Replies
  1. POWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

   Delete
 17. LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA
  LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA

  LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA LOWASA

  ReplyDelete
 18. Mdau hapo juu umekomesha hizo LOWASA mie hoi. pipoooooos power

  ReplyDelete