asas

asas

sintah

sintah

SIKU ZIMEBAKI 30 NA MAMBO NI MAZITO


Taasisi ya TWAWEZA yatoa ripoti kwamba Magufuli atashinda kwa kishindo kikubwa je unaamini hilo ama unalionaje?

ila Taasis hiyo imezua balaa baada ya watu kohoji maswali hapo  chini hebu yasome na kisha na wewe utoe maoni yako......

Maswali 14 yaliyoibuliwa na tafiti ya Twaweza:


1. Kwa mara ya kwanza Twaweza walisoma ripoti ya utafiti na kuonyeshwa moja kwa moja na TV. Nani alidhamini utafiti, matangazo hayo na kwa madhumuni gani?2. Kwa nini waliamua kutoa matokeo ya utafiti wao katikati ya kampeni zenye ushindani mkali na mhemko mkubwa wa kisiasa?3. Je, ni jinsi gani watu waliohojiwa walichaguliwa?4. Je, watu waliohojiwa ni wa kutoka maeneo gani, makundi gani ya watu, ukiacha jinsia?5. Je, waliohojiwa wamejiandikisha kupiga kura, mashabiki tu au mchanganyiko?6. Twaweza wanajua kwamba kampeni za wagombea urais huanza baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuidhinisha wagombea waliopendekezwa na vyama. Kwa nini shirika hilo lilianza kufanya utafiti siku mbili kabla ya hapo?7. Twaweza wanasema wahojiwa hawakupatiwa orodha ya majibu ya kuchagua. Je, ni kweli hawakuwa wanawajua wagombea wengine waliotajwa zaidi ya Dk John Magufuli na Edward Lowassa wakabaki kusema “mwingine?”8. Katika nafasi ya ubunge na udiwani, wahojiwa wameonyesha kuwajua na kuwapigia kura wagombea wa ACT-Wazalendo. Inakuwaje watu hao hao washindwe kumtaja mgombea urais wa chama hicho badala yake Twaweza ikamweka katika kundi la “mwingine?”9. Takwimu zote asilimia huwa ni 100 iliwezekanaje mgawanyo wa takwimu katika ripoti ya Twaweza katika baadhi ya maeneo asilimia zilizidi na au kupungua 100?10. Tafiti zilizopita za Twaweza zilikuwa zinajumuisha watu wengi na zilikuwa zinaonyesha mtu aliyeshika nafasi ya kwanza pengine hadi 10. Kwa nini katika utafiti huu waliwalenga wawili tu Lowassa na Magufuli?11. Ripoti inasema kwamba dodoso la utafiti huu liliandaliwa kabla ya uteuzi wa wagombea urais wa vyama vingine (nje ya mseto wa Ukawa), kikiwamo ACT-Wazalendo. Je, dodoso hilo lilikuwa na maelekezo gani kiasi kwamba ikawa vigumu kuwaingiza wagombea wengine?12. Kwanini matokeo ya utafiti na kinachoonekana nje ni picha mbili tofauti?13. Matokeo ya awali ya Twaweza yalionyesha Lowassa alipokuwa CCM aliongoza kwa ushawishi, iweje ndani ya wiki mbili baada ya kuhamia upande wa pili aporomoke hivyo?14. Kwanini Twaweza hawakushirikisha Zanzibar katika utafiti wakati urais ni wa Muungano?


16 comments:

 1. OOT:Thank mdau wa trh 22,2015 at 1:39...ulisema nikuandikie email yangu kwa ajili ya IVF costs...the email is : lizyd54@gmail.com. Mungu awabarik sana wadau wa blog hii tusaidiane jaman.Nawatakia ijumaa njema.

  ReplyDelete
 2. MIE NAAMINI ATASHINDA KWANI
  LOWASA ALISHA FANYA MAKOSA NYUMA
  LOWASA KATUONESHA SI MWAMINIFI HUWEZI KUHAMA CHAMA KISA HUKUCHAGULIWA KUGOMBEA RAISI KWANI WANGAPI WALIKUWEMO KWENYE LISTI.
  SIDHANI KAMA LOWASA ANATAKA KUWAONGOZA WATANZANIA NAAMIN ANATAKA MADARAKA NA PESA KUPITIA SIASA.

  MASWALI MENGI SINTAH UNGEKUJA NA MAWILI MAWILI USHANICHANGANYA KABISA
  NAHIVI SIPENDI SIASA BASI NTARUD BAADAE DARASANI KWAKO

  ReplyDelete
  Replies
  1. Wewe inaonekana mama wa nyumbani, Sasa hivi ni mabadiliko time huku makazini tunakatwa Payee kubwa sana napata uchungu kuona hela inakatwa afu hamna maendeleo,nsahfika Rwanda nchi ndogo sana iliyopata uhuru miaka mingi baada yetu lakini wako mbali sana kimaendeleo,miundombinu na afya ila sisi hamna kitu.
   Rushwa imezonga sana nchi yetu lazima ujuane na mtu upate haki yako.
   Mfano hai: Wizarani hapa kuna zabuni zillitangazwa shirika ambalo lilipita kwa haki likawa lipewe zabuni lakini ilipigwa simu moja kutoka kwa Ridhiwani Kikwete yule mtoa zabuni akaambiwa aipe kampuni nyingine isiyo kidhi hata vigezo haina vifaa wala nn ila ndo akapewa zabuni.Je?kwa mtaji huo kutakuwa na maendeleo,Barabara mbovu,Hospitali mnalala watu wawili,maji hamna,umeme ndo msiseme elimu ndo hoiiii chalii.
   Kwangu mimi kura yangu inaenda upinzani kwa kweli uaminifu siangalii maana yy sio mchumba wangu nataka uadilifu.
   kama mnakimbilia uaminifu kwa magufuli muulizeni alikuwa muaminifu kwa mkewe?na yule mke mdogo wa kebby's vp????????????????????????????

   Delete
  2. wewe acha dharau zako, kwani mama wa nyumbani hajui maisha ni nini? Hao watu wenu wamecontribute kwa kiasi kikubwa kwenye matatizo ya nchi hii. Wewe mwenyewe mmoja wapo, uko kazini, unatumia muda wa mwajiri kuangalia mitandao na kuandika mi comment yako ya kijinga na ni majority humu, wkends huoni kama mitandao iko kimya? wote ni wafanyakazi, wezi wa muda wa mwajiri, acheni ujinga, kuto kufanya kazi kwako ndo kumeleta matatizo, halafu unajifanya mabadiliko.

   Delete
  3. Nimekupenda bure shosti, japo hujui siasa, lakini una akili ya kupambanua, achana na haya manyumbu

   Delete
  4. Muda wa muajiri hii serikali yetu hii ndo unaita mda muajiri,wao wanakata kodi na hawaleti maendeleo je pia nao si wezi?? bora mie nnaeiba mda badala ya kuiba hela na jasho la mtu.
   Una uhakika mm sifanyi kazi kazi nafanya sana tu ila mwisho wa siku inatoka amri ya mtu mwingine hiki kifanyika kingine nchi mmeigeuza duka la mangi,weekend kwako labda ndo kuko kimya kwa speed ipi ya serikali uingie mtandaoni siku hizi hadi wamasai wana smart phone weekend or weekday macho kodo humu na simu yangu Tecno or not si inashika network bana Nyie Manyumbu ndo tumewatoa jasho mwaka huku Mabadiliko!!!!!!

   Delete
  5. Imekutouch sana naona ANONYMOUS 3:29AM au ww Maza House teh teh teh teh teheeee bwahahhahahaahaaaaaaaaaaaa

   Delete
  6. Mi na Familia yangu tutachagua Lowassa Tu CCM OUT TUMECHOKA

   Delete
  7. Mama wa nyumbani wewe dada niko serekalini nakula kwa naksh baki ukawa usubiri waajiriane kindugu mwisho ndo wewe

   Delete
  8. Uaminifu wa nini sasa kwani chama ni mama/baba au mume/mke maana hata hiyo siyo ishu sana maana mke au mume akizingua ktk kiwango ambacho hakivumiliki ndoa inatenguliwa na wazazi pia hawapaswi kusikilizwa ikiwa wanafanya upotoshaji

   Delete
  9. Anony wa 5:43 AM usiusemee moyo wa mtu, hata kama ni mwanao, chumba cha kupigia kura anaingia mmoja tu, mimi mpenzi wangu yuko kile chama cha wafujo na vurugu, imebidi nijifanye namsupport, ila siku ya kura najua nampa nani, so pole were unaesema mi na familia yangu,

   Delete
 3. kwa mara ya kwanza umeandika kitu cha maana. kama kweli una masters unatakiwa kua level hizo au umecopy mahali

  ReplyDelete
 4. KWELI MDAU HAPO NAKUUNGA MKONO! AKINA MAMA WA NYUMBANI WANATUANGUSHA SANA. WAO HAWAJUHI MACHUNGU YA KUTAFUTA. WAO AKINA MAMA HAWAKOSAGI KWENYE MIKUTANO/VIDEDEA VYA CCM. NA UKIMUULIZA HIVI KWANI UNAKIPENDA CHA CCM? HANA HOJA YOYOTE YAKUKUJIBU. KURA YANGU ITAENDA KWA LOWASA/UKAWA.

  ReplyDelete
 5. Nimekupenda bure 1;16

  ReplyDelete
 6. wifi yako wa taifa zima zari karudi kwake
  esma nyumba ni yako mamy chagua pa kumlaza mwanao sasa

  ReplyDelete
 7. lowasa ndo ntampa kura yangu haijalishi amehama au amefanyaje chamsingi ni mabadiliko na kuuambia ulimwengu kwamba tanzania sio fisiem. suala la uaminifu ni kwenye ndoa na sio uongozi wa nchi!

  ReplyDelete