asas

asas

sintah

sintah

KINGUNGE NGOMBALE MWIRU AJIOTOA CCM


KADA wa siku nyingi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru ‘ametoroka’ chama hicho kutokana na kile alichokieleza kimepoteza mwelekeo.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake leo jijini Dar es Salaam Kingunge amesema, hatojiunga na chama chochote cha siasa “lakini kuanzia sasa mimi sio mwanachama wa CCM,” amesema.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, neno ‘mabadiliko’ lilitawala kinywa chake huku akionya kuwa, nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa.

“Nguvu ya kupinga mabadiliko ni kubwa sana lakini kwa utafiti wangu mimi mzee ni kuwa, nguvu ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi. Watu wajiamini zaidi na wasubiri tarehe 25 Oktoba mwaka huu,” amesema.

Akielezea namna CCM ilivyopoteza mwelekeo Kingunge amesema chama hicho kimelewa madaraka kutokana na kutawala kwa muda mrefu na kuongeza kuwa ‘wananchi sasa wanataka mabadiliko.”

Hata hivyo, kiongozi huyo aliyejiunga na TANU siku saba baada ya kuanzishwa kwake na baadaye TANU na ASP ya Zanzibar kuungana na kuanzisha CCM mwaka 1977 amesema chama hicho tayari kimeishiwa pumzi.

“Kuongoza nchi ni kama kupanda mlima, utafika mahala pumzi zinakwisha na huwezi kuendelea mbele na ukijaribu kwenda mbele unabaki pale pale, na hivi ndivyo CCM ambapo kimeishiwa pumzi na kimebaki pale pale hakiwezi tena kupanda mlima,” amesema Kingunge.

Baada ya kutangaza uamuzi wa kujiondoa CCM, amesema hakusudii kujiunga na chama chochote, Kingunge ameeleza kuwa alipigana ndani ya CCM kutaka kuhakikisha chama hicho kinabaki salama kwa kumchagua ama kumpitisha mtu aliye na sifa na kukubalika.

“Nilipigana nikiwa ndani ya CCM kuangalia nani anafaa ili kuileta nchi kwenye mstari. Niliangalia ili kujua ndani ya chama nani tukimpata anaweza kuipeleka nchi mbio.

“Nilimwona Edward Lowassa kuwa ana sifa kuliko wengi waliojitokeza. Kiongozi lazima akubalike na watu, hii ni sifa tangu wakati wa TANU,” amesema Kingunge na kuongeza;

“Lowassa anakubalika ndani ya CCM na nje ya CCM, ni hivyo pamoja na kutangaziwa mambo ya ajabu kwa miaka minane mfululizo.”

Lowassa ambaye alihama CCM na kujinga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alipitishwa na chama hicho kuwania urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Chadema ni miongoni mwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ikiwa ni pamoja na Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

Kabla ya kujiunga na chama hicho, ndani ya Serikali ya awamu ya nne, Lowassa aliwahi kuwa Waziri Mkuu ambapo alijiuzilu nafasi hiyo kutokana na kuhusishwa na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Pia Kingunge ameshngazwa na hatua ya CCM kutoa kauli zinazoonekana kung’ang’ania madaraka.

Amesema “kauli zinazotoka sasa hivi, wapinzani hawawezi kushinda. Nyinyi mnajuaje kama hawawezi kushinda? Ukiritimba wa chama kimoja kwa karne moja umetosha, madaraka hulevya.”

Akizungumiza chama tawala kuacha utamaduni wake Kingunge amesema chama hicho kimeacha ‘itikio’ lake lililoasisiwa tangu kuanzishwa kwa chama hicho.

“Wamebadilisha kauli mbiu ya chama badala ya kidumu Chama Cha Mapinduzi – kidumu, sasa wanaitikia kidumu chama tawala,” anasema na kuongeza; “niliwaambia NEC kwamba ukisema hivyo maana yake wewe unataka kubaki kwenye utawala.”

Akimzungumzia mgombea urasi wa CCM, Dk. John Magufuli, Kingunge amesema nafasi hiyo ameipata kutokana na chama hicho kuvunja katiba ya chama.

Hata hivyo ameeleza kuwa, tatizo kubwa la wananchi ni uchumi na ajira, “umasikini uanondolewa na uchumi bora,” amesema.

Amesema, Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa aliacha uchumi ukikua kwa asilimia saba na kuingiza nchi kwenye orodha ya nchini zinazokwenda mbio kiuchumi.

“Tazama, Kikwete (Rais Jakaya Kikwete) kapokea uchumi ukikuwa kwa silimia saba na sasa ni miaka 10 uchumi unakuwa karibu na asilimia saba -miaka 10 hii yote tumepiga make time na kiukweli tumerudi nyuma. Mabadiliko ni muhimu ili upate watu wengine wenye pumzi mpya,” amesema.

8 comments:

 1. mm yeye ndo kapoteza mwelekeo na kama CCM imeishiwa pumzi basi na yeye anaenda sambamba nayo au yeye ndo kaishiwa pumzi zaidi ya CCM coz yeye CCM imemkuta. Ana hasira za kukosa sehemu za kuponea njaa. Ubungo waalee ataisikia hewani. Nilikuwa namuona wa heshima huyu mzee saizi naona anajishusha ka suruali ilokosa mkanda. em akapumzike uko awaache wenye meno yao wavunje mifupa. kwahiyo huyo Lowassa angekuwa CCM ndo ingekuwa haijaishiwa pumzi? makuubwa! mi namuona ana hasira tu za kukosa pa kula.

  ReplyDelete
  Replies
  1. khaa yaani kingunge huyu huyu amekosa pa kula?????? seriously???? aysee wewe utakuwa mgeni nchi hii au hujui choochote kuhusiana na siasa za Tanzania.

   Delete
 2. huyu mzee kaishiwa cha kuongea , angeondoka kimya , kimya bila kukisifu wala kukashifu akasema tu nimeamua kustaafu atlist ningemwelewa, lakini maneno mengi wakati yeye mwenyewe alikuwa ndani ya urudishaji nyuma wa maendeleo ya Tanzania , nani aisyejua we mzee kaa utulie na ukitaka kuhamia chama chochote ni ruksa so baada ya kulaaaaa ndo mnaona chama hakifai , kweli mzee umeishiwa pumzi.

  ReplyDelete
 3. Kabisa ana stress huyu mzee,apumzike tu sasa...hana jipya

  ReplyDelete
 4. Mimi sioni kama ni busara kuwaponda watu baada ya kujitoa kwenye chama, kama wana matatizo wawe wanawajibishwa siyo kusubiri hadi wajitoe ndiyo tuhuma zinapamba moto

  ReplyDelete
 5. Busara zake ampelekee mwanae anaeua watu kwa madawa ya kulevya. Kama kweli anajali welfare ya nchi angemkataza but yeye ndio anamlinda kila siku. Pleae tunampa Magufuli because of people like him. Wanafki wote muondoke ccm mutuwache kabisa.... Ccm juu

  ReplyDelete
 6. Fisiem yakuburuza wananchi,wachache wale wengi waumie idiots r.I.p ccm wanaoshabikia ccm wamelogwa na aliewaloga kafa kupona hawawezi kupona endeleeni kuwa wafungwa katika ujinga wenu.may yr soul rest in hell ccm

  ReplyDelete
 7. Anney umenifurahisha sana!! agiza chochote nitalipa hahahaaaa, kweli kabisa wamelogwa hawajitambui RIP Fisiem!! someni alama za nyakati, vijana wameamka ni wachache waliosongwa na mawazo mgando kama nyie hapo juu. Viva Lowasa, asante mzee Kingunge kwa kueleza ukweli.

  ReplyDelete