asas

asas

sintah

sintah

HAPA KAZI TU.........

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Christmas na Mwaka Mpya kwa gharama za serikali/umma, kwa mwaka huu.

Balozi Sefue, ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo, afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.

Badala yake Balozi Sefue ameagiza fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara na Taasisi za umma zinadaiwa na wananch/wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
26 Novemba, 2015

3 comments:

  1. Sipati picha km hii ndiyo ingekatazwa wkt wa JK uwiiii,wananchi wangesema analeta udini na mapovu yangewatokaje kwa mfano,bado mwenge nao ufutwe,Big up JPM,sidhani km kunahitajika mawaziri mimi naona km wao wanatosha na wakuu wa mikoa bila kumsahau Makonda umetisha

    ReplyDelete
  2. hizo pesa zitapelekwa kweli huko wanakosema??whats wrong with kuchapisha kadi kwa gharama za serikali? Mbona bungeni wanapewa posho kwa gharama za serikali wapige marufuku na hili pia..

    ReplyDelete