asas

asas

sintah

sintah

WATANZANIA TUNAENDA WAPI?

RIP Mawazo
mauwaji ya kinyama
Ni habari za kusikitisha sana kwamba ndugu zetu wanauwawa kwasababu ya siasa, jamani amani  na upendo tuliokuwa navyo vimetoweka wapi? RIP ,Mawazo, mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, ameuwawa kikatili kwa kuchinjwa chinjwa kama kitoweo...

11 comments:

 1. Hivi siasa kwanini ni uadui? mwanasiasa yupo tayari kuteketeza taifa ili aongoze miti sijui ilimradi tu awe madaraka! kiukweli wanasiasa wa namna hii hawana jipyya wala hawana nia njema na taifa ushirikina na uadui na ubinafsi ndo umewajaa ila vita si yetu ni ya Mungu, Mungu wa kisasi akaonekane juu ya aliyetuma watu wakatoe uhai wa baba huyu.

  ReplyDelete
 2. Hilo neno kuchinjwa kama kitoweo lina ukakasi mkubwa sana na halipendezi na kwa ndugu jamaa na malafiki naomba ubadilishe hilo neno

  ReplyDelete
  Replies
  1. kweli mdau na hiyo picha ya hospitali sintah itoe inaumiza kuangalia

   Delete
 3. roho yake inamlilia Mungu! damu yake itakuwa juu ya yeyote aliyehusika kwa namna yoyote kwa mauaji!

  Jamani dunia ni mapito kumbuka wangapi walikuwa viongozi na leo hatunao wametangulia mbele ya haki? kumbuka kuna maisha baada ya maisha haya, tumuogope Mungu! kwa nini ukawa jamani? Mungu tuokoe

  ReplyDelete
 4. hakuna atakayetawala milele ila Mungu peke yake!

  RIP ndg

  ReplyDelete
 5. Ni matokeo ya siasa za chuki na visasi. Tunaweza kutofautiana kimtizamo na kiitikadi lakini bado tukaendelea kuheshimu na kuthamini utu wa mwanadamu. hii ni fedheha kubwa sana R.I.P Brother!

  ReplyDelete
 6. Mungu amewaona na atawahukumu kwa unyama huu. Amen

  ReplyDelete
 7. Ndio maana kwenye mada iliyopita nilimwomba Mheshimiwa JPM atoe tamko la kuwakanya watu wanaojiinua na kujiweka daraja la juu katika nchi! kisa yupo chama fulani!!! matokeo yake ndio kama haya watu kujichukulia sheria mkononi!!! ni hatari sana hii.

  ReplyDelete
 8. Mwanza kwa wasukuma musoma kwa wajita wakurya maeneo ya ziwa ni wakatili kutoa roho ya mtu kwao sio shida, abari za kuua wachawi wao kukata mapanga vizee wao,viungo vya maalbino wao wamezaliwa makatili, Raisi Magufuli kaanze kazi ya kusafisha mkoani kwako

  ReplyDelete
  Replies
  1. Acha urongo wewe! Senkondo, mwandishi mbeya, Ulimboka, n.k.n.k . ni Mara au Mwanza!? hizi ni sababu za kisiasa wenyewe wanajijua wanaofanya hivyo cha msingi waache mara moja. Maana anaeua kwa upanga atakufa kwa upanga. Period

   Delete