asas

asas

sintah

sintah

WATEJA WA AIRTEL KUTUMA PESA BURE.....
Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando alisema " kwa mara nyingine tena tunadhirisha kwa vitendo dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu, rahisi na zenye gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel Money. Leo tunawawezesha wateja wetu wa Airtel money nchi nzima kuokoa pesa wanapotuma pesa kwenda kwa mtumiaji wa Airtel kwani tozo za kutuma pesa ni BURE kwa kiasi chochote kitakachotumwa. Tunaamini ofa hii ya "Okoa Mapene'' itakuwa kichocheo kikubwa kwa wateja kutumia huduma ya Airtel Money kwa muda wa mienzi mitatu na zaidi"
Aliongea kwa kusema "Okoa Mapene'' ni njia mojawapo ya kuwazawadia wateja wetu wanaotuma pesa kwa ndugu , jamaa, marafiki, familia na washirika wao wa biashara kupitia huduma ya Airtel Money. "Okoa Mapene'' pia kuwawezesha mawakala kupata kamisheni zaidi kutokana na kuwa na wateja wengi watakaofanya miamala mingi kuanzia sasa.

Ili kupata kutuma pesa mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa kwenye menu ya Airtel Money na kuanza kufanya miamala yake BURE.Hiv karibuni Airtel imewazawadia wateja wake kwa kuwapatia gawiwo la faida watumiaji wote wa huduma ya Airtel Money na kuwawekea gawiwo hilo moja kwa moja kwenye akaunti zao za simu.2 comments:

  1. Halafu Sintah, hawa airtel wako waambie waache kutukata pesa zetu bila sababu, uchumi wenyewe mbovu halafu na wao wanatugandamiza lo!! Yaani mtu unaweka kavocha kako may be saa tano na nusu usiku, halafu hujakatumia hata kidogo ila umejiunga unaamka hasubuhi unashangaa kamekatwa!!! ndio nini sasa, washatufanya watz chuma ulete wao eeeh!!? Kingine unajiunga na bando la airtel kwa ajili ya Internet nakwambia hako kaspidi mbona utakomaaa yaani kila kitu hakifunguki kuanzia Sintah, facbook na wengine woote mpaka kapesa kote kanakwisha mtandao haupatikani lo!!!! waambie wajirekebishe bwana da... Au tuwasemeee kwa mhe. wafanyiwe surprise kama muhimbili!!!

    ReplyDelete
  2. Kwa airtel gani? Uliza mawakala hatulipwi commision hata miezi miwili utafatilia hadi uchoke. Ukikosea kutuma hela ndio imekula kwako. Nshamtumia mteja laki 6 na nusu katika kutuma akawa anachanganya pin ya line 1 na 2ikafungwa akaomba nipige airtel wakasema wanairudisha kwangu means yule hatoitoa tn ht kama pin atapewa. Ilikuwa asubuh saa 3 akarudi jioni saa moja nikamwambia ajaribu kutoa eti ikatoka Kwhy hawakuizuia ina maana line ilojiblock haikuwa airtel mteja hukujua.Na airtel nao hawajui ht line ka imejifunga au lah. Je ningekuwa nimekosea namba na nawategemea airtel wairudishe kwangu si ningekoma laki 6!!! Wanaboa kichiz hao

    ReplyDelete