asas

asas

sintah

sintah

AIBU YA KUFUNGULIA MWAKA......Haaa waswahili wanasema baniani mbaya kiatu chake kizuri, hivi TFF na uongozi mzima wa maswala ya michezo Tanzania walimshobokea Samatta na kuwaacha wazazi wake wakimsubiri mtoto wao katika ngazi za Airport kaaaa mmetutia aibu ya mwaka jamani kama sio wazazi wake kumlea katika maadili na kufika hapo leo mngemuona huyo Samatta? hivi ni u selfish wa aina gani mupende boga na msipende ua lake? hivi unajua nidhamu unafundishwa na wazazi wako kama wasingemfundisha nidhamu ya kuwa na adabu katika kazi leo mngemsikia wapi huyo mbwana yaaani TFF muwaombe radhi wazee wa Samatta, walipaswa wawe VIP kuna mijiti mingapi inajazana VIP wasio na mbele wala nyuma kwanini hamkuwapa wazazi kipaumbele? ni sikitiko la taifa...

4 comments:

 1. NDO SHIDA YAO HAO MAFALA, KAZI KUSHOBOKA TUU NINGEKUWA MBWANA NINGEWACHUNIA KWANZA HADI NIWAONE WAZAZI WANGU. SASA HIVI KILA MTU ATAKUWA ANAJIDAI ANATAKA KUWA KARIBU NAYE HASA ZILE REDIO ZETU WANPENDA SANA KUJISHEUA NA JUHUDI ZA WATU WENGINE. MFYUUU… SASA NA YULE ANAEBADILI WANUME KAMA NGUO HUYU NDO TAGETI YAKE KWA SASA LAZIMA JAMAA ATALAMBA TUU MANAKE TUSHAANZA KUJILENGESHA IDRISSA ASUBIRI KUPANGWA KAMA DIAMOND! NAWAPA MIEZI MITATU TUYA KUMWAGANA.

  ReplyDelete
 2. Ni kweli walifanya vibaya sana kama kweli waliwaacha wazake wa Samanta wakishangaa airport, sio haki wala heshima kwa kweli TFF fanya jambo juu ya hawa wazazi.

  ReplyDelete
 3. Ni aibu tupu maskini pole yao

  ReplyDelete
 4. KWA MARA YA KWANZA UMEONGEA POINT

  ReplyDelete