asas

asas

sintah

sintah

HONGERA SANA SALMA KWA KUPATA BABY BOY

Mungu ndio kila kitu

new mom in town
Mungu anampa mja wake kitu anachokiomba na kukitaka katika wakati Mungu anaotaka yeye, hivyo ndugu zangu ambao hamjapata watoto endeleeni kuwa na subira.... hongera sana Salma na mtoto wako Mwenyezi Mungu akkukuzie na kukulinda

40 comments:

 1. hongera sana salma

  ila kaswali kwan danish hakuwa mwanawe??

  ReplyDelete
  Replies
  1. Danish ni mtoto wa dada yake...kweli alimpenda mno danish hadi mungu kampa wa kwake...ushauri kwa wamama wanaotafuta watoto jamani jitoeni kwa watoto yatima kwa mioyo yenu na watoto wote less priviledged maana sala zao huenda moja kwa moja kwa mungu na mungu atawapa watoto mimi nimeona mtu aliefanya hivi na mungu hakumtupa pamoja na sisi kusali wenyewe pia sala za hawa watoto yatima zina uzito

   Delete
  2. umenenea mdau mimi nilitafuta sana mtoto kwamiaka 15 madoctor wote bora niliwaendea, ivf nilifanya 5 zote zikadunda nikaona basi hakuna namna nikasema naenda kuadopt nikafunga mjadala wa kuhangaika kwa madaktari yani haikupita miezi sita nikabeba mimba tena natural nikazaa nikiwa 38 mtoto ana miaka mitatu sasa.
   ni kweli mara nyingi sana watu ambao wana adopt kwa moyo mmoja huwa wanafanikiwaga tena ghafla saa nyingine kabla hata hujapewa huyo mtoto.

   Delete
  3. Ameen
   Kweli swala za Yatima zinapokelewa.
   Ila wanawake tuoendane ili mema tuombeane.
   Mungu akikupa ,Akikuchekeweshea au asipokupa kabisa ni mapenzi yake,
   Vidole havijafanana na maisha yako tofauti

   Mungu awape watoto wote ambao hawana au wanatamani
   Wawe wtt wema na wenye baraka
   Hongera mdada karibu ktk ulimwengu wetu wa kulea
   Mungu pokea maombi yetu wabariki wanawake wenzetu

   Delete
  4. Daaah, kweli mawazo ya mwanadamu sio ya Mungu;Mungu ni mwema sana sana;na anatenda kwa wakati wake ..cha msingi ni kuwa na imani; nakumbuka Salma Msangi ameolewa miaka mingiiii;kumbe alikuwa hajabarikiwa? daaah UTUKUFU kwa Mungu...

   Nawapa moyo wanawake woote wanaotafuta motto,wasikate tama,Mungu anatenda kwa wakat na majira yake ,tusilazimishe-mfano mzuri ni huu hapa kwa Salma Msangi..Nina wa Kaole naye alikaaa miaka kumi bila motto; Mungu akaja kumpa mapacha watatu kwa mpigooo;aaah Mungu ni mwaminifu sana sana

   Delete
 2. Amen. Hongera sana na Mungu akujalie uzima na furaha tele katika maisha yako.

  ReplyDelete
 3. Ameen
  Inshaaallah Mola awafungulie wote walotani watoto au walochelewa kupata.
  Kwani mapenzi ya Mungu na msamaha wake ni mkubwa Kuliko kashfa zetu za Kuwaita watu WAGUMBA
  MUNGU anatupenda sana
  EE MOLA WABARIKI WANAWAKE WOTE NA UWAPE WANACHOKITAMANI MIOYONI MWAO WEWE NDO MUWEZA WA YOTE

  ReplyDelete
  Replies
  1. AMEN. MUNGU AKUBARIKI WW ULIEANDIKA HII COMMENT.

   Delete
  2. Ameen uloniombea Dua
   Inshaaallah Mola atawapa wepesi wote walochelewa kupata .
   Hakuna zito wala linaloshindikana kwa MUNGU
   Ktk swala zangu nawaombea wanawake wenzangu wapate wanavyovitamani na wapolelewe maombi yao.
   MUNGU awape wepesi ktk nyumba zao na wanaozitamani ndoa WAPATE zenye faraja na furaha
   Wanawake tuombea dua .

   Delete
  3. aallahum aamin

   Delete
 4. Hongera sana Salma, i wish kama angeshare siri ya mafanikio yak e ingeasaidia kwa wanawake waliochelewa kupata watoto, God bless her and her Son

  ReplyDelete
  Replies
  1. siri kaachana na mume wake na kapata mtu mwingine- hata wanaume wanakuwaga wagumba!

   Delete
 5. Nasikia watu walimuita huyu dada majina yote kisa tu hana mtoto
  Hakika kila mja na ridhiki yake
  Hongera mama

  ReplyDelete
 6. Kila jambo na wakati wake,MUNGU ashukuriwe sana

  ReplyDelete
 7. Mtaa wa pili kumedoda madai yake anatengeneza shape kwanza. Mmmh kukosa sponsorship kuna tabu jamani.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kumbe unakutamani eeh?

   Delete
  2. ni kweli kumedoda kwani uongoo? shape ipi sasa kufulia january ni kawaida ila watu hawakubali sijui kichwa panzi atamaliza lini likizo yake.

   Delete
  3. mi naona anaepata presha ni yule mwenye post ya juu. Kwasababu kuna comments bado hazija pitishwa. Yaani kaachwa roho juu..ni mateso hayo. Na anavokuwaga busy kuwajibu watu sijui atakuwa kajiandaaje..loo!

   Delete
 8. Sinta Mbona humsifiii Wema kuwa mjamzito?

  ReplyDelete
 9. OOT: Usiombe ukaolewa halafu mimba haingii halafu kazi unatafuta hupati utajutaaaaaa,dunia utaiona chungu,matusi utakayotukanwa every blame on u, kama mambo ya mume hayaendi vizuri mume anaanza kuona kma ameoa mkosi anatafuta mchawi usiombe ndugu zangu yawakute, mengine siwez kusimulia

  ReplyDelete
  Replies
  1. Yanatokea kwa wasio kuwa karibu na Muumba tu na uswahili mwingi
   Vitu vingine hata wataalamu hawawezi ila kazi ya Muumba tu.
   Kuna mwanaume alikosana na mke kisa anazaaa watoto wakike akamwapiza
   USIPOZAA WA KIUME NDO TALAKA YAKO'
   Na mwanamama Akazaa wa kike wakawa wtt 4 wa kike.
   Akamtenga mkewe akaleta chomba kipyaa
   Mke mdogo akajaaliwa mtt wakiume .
   Mtoto alizaliea na kilema . Ee MUNGU tunusuru
   Hapo ndo tunaoneswa UFALME wa MUNGU ulivyo
   Tuwapmbee baraka wanaotafuta watoto na MUNGU awape watoto wenye usikivu na maadili
   Mungu wajaalie wanawake wenzangu wape kapo kamoja tu

   Delete
  2. Nilikaa kwenye ndoa yangu ya kwanza kwa miaka 8 bila mimba,mbaya zaidi nilikuwa nakaa na mama mkwe(mlemavu)kwani mume wangu ndio alikuwa mtoto wake wa kiume peke.Basi mawifi wakija kumuona mama yao ni mafumbo(vijembe)mbaya zaidi hata mume wangu alikuwa hajali wala kuwakemea,mwisho nilinyosha mikono nikaondoka,mume akaoa mke mwingine,na mimi nikapata mume mwingine,nina watoto wawili wa chapchap,yeye mpaka sasa hajajaliwa.Tumuache Mungu aitwe Mungu binadamu hatuna sababu ya kudhani.Najua watasoma hapa japo sijataja jina.MUNGU AWABARIKI WANAWAKE WOTE.

   Delete
  3. Nimesoma coment yako nimehis kam mchoz unitoke kwel mungu wa ajabu umepata watt wawil na mume mpk sahz hana wanaosema malipo hapa hapa dunian hawajakosea,nawaombea wanawake wote mliopo kwenye mahangaiko ya kupata mtt mungu na awafungulie amen


   Delete
  4. Yan,wakat mwingine tatizo ni kwa mwanaume,lakini watanzania ndo tushazoeaaaaaa kulaumu wanawake,saivi wanaume wengiii mbegu hazina nguvu,mimba iotaingiajeeeeeeeeeeeeee

   Delete
  5. Amina namimi ntapata mniombee.

   Delete
 10. Amina! Hongera Salma Mola ampe maisha marefu.

  ReplyDelete
 11. Hongera sana Salma,Mungu wetu awe nawe katika kukuza dume lako.

  ReplyDelete
 12. mwenzenu nipo kwenye ndoa mwaka wa 3 sasa nasaka mtoto simpati, basi nikisoma masumbuko ya watu ambao hawajajaliwa roho inanidunda naogopa vibaya mno, japo mume wangu yuko very supportive and loving hata familia yake haina shida ila najiuliza nikiendelea kuchelea kupata huyo mtoto vituko vikaanza sijui ntafanyaje mie, na hivi kuongea sijui, Mungu ananinusuru

  ReplyDelete
  Replies
  1. Keep on praying,Mungu anatenda kwa wakati wake,si unaona mfano wa Salma Msangi,Nina..Name nakupa ushuhuda,rafik angu aliolewa 2008;kaja kupata motto 2015 after 7 years..Watu before walisemaaa weeee,hadi wakamwambia mume azae nje,lakini Mungu alivyo na mipango yake?thubutu hata hyko nje hakupatikana,saiv ana kabint kake ka mwaka mmoja.. Mungu sio mwanadamu,mawazo yertu sio mawazo yake,anatuwazia yaliyo mema

   Delete
  2. Dear utapata tu mtoto kwani Mungu yu mwema siku zote,sali,usinyanyase,fanya matendo mema kama Mungu mwenyewe alivyotuagiza kupitia kwa mitume wake,nami ninakuombea,naamini muda si mrefu utakuja kutupa ushuhuda.MUNGU AKUBARIKI.

   Delete
  3. Amen, Amen, Amen

   Delete
 13. alafu nimependa ambavyo hakufanya matangazo, manake wengie tumejua baada ya kuwa amejifungua tena baada ya kuanza kupewa hongera, angekuwa mwingine hapo na hivi alichelewa kupata loh wangemkoma. Hongera sana sana tena sana, i hope na mimi siku moja Mungu atanikumbuka na wale wote watafutao

  ReplyDelete
  Replies
  1. Umeona eeh,wengine kuanzia mwezi wa kwanza ni vituko,
   mimba inakuwa na matangazo utadhani harusi.Ngachoka!

   Delete
  2. Tunamuombea na Mishi Bomba nae apate wake,miaka mingi imeenda,nkikumbuka ile kitvhen party,yale mafenichaaa

   Delete
 14. Amen wadada wazuri Mwenyezi Mungu hutoa kwa wakati wake na tuzidi kumwomba na kumtegemea siku zote.

  ReplyDelete
 15. ehh muumba wetu tusaidie na kutukuzia watoto wetu ktk maadili mema na uwajaalie wasiopata nao wapate kwa fadhila zako kwani hakuna kubwa kwako..congrats Salma

  ReplyDelete
 16. Hongera sana da salma, mungu yu mwema na tujifunze kitu kupitia kwake kwani hatunaga subrah.

  ReplyDelete
 17. Jamani nisaidie mimi nataka kuadopt motto naomba mnielekeze utaratibu wa kufuata. maana sijui hata nianzie wapi. mungu awabariki

  ReplyDelete