asas

asas

sintah

sintah

RAIS JPM AFANYA UTEUZI WA WAKUU WA MIKOA....

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
 
Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
 1. Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
 2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita.
 3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
 4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
 5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
 6. Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
 7. Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
 8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
 9. Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
 10. Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa wa Singida.
 11. Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
 12. Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
 13. Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
 14. Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa Mkoa Dodoma.
 15. Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
 16. Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
 17. Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa Mbeya.
 18. Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa Mwanza.
 19. Mh. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
 20. Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
 21. Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
 22. Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
 23. Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
 24. Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
 25. Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
 26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Machi, 201

4 comments:

 1. HONGERA SANA JPM KWA KUMTEUA PAUL MAKONDA KUWA MKUU WA MKOA WA DSM. MAKONDA NI KIJANA SHUPAVU, MBUNIFU, MFUATILIAJI KWA KIFUPI ANAJITUMA. TUNAMUOMBA MH. MAKONDA JIJI HILI LINA MAMBO MENGI AMBAYO HAJAKAA SAWA KWA MFANO: UCHAFU NI MWINGI SANA HASA UKIENDE MAENEO YA SOKONI KAMA VILE SOKO LA BUGURUNI. PIA KERO YA HAWA OMBAOMBA WALIOJAA BARABARANI MAANA UKISIMAMA TU MWENYE FOLENI WANAKUZUNGUKA MADIRISHANI WAKOMBA UWAPE PESA SI WATOTO WALA SI WAKUBWA. NA OLE WAKO UKIWANYIMA WATALIPIGA KIOO CHA GARI LAKO. KWA KWELI NI KERO. NAOMBA UFANYE MPANGO HAWA OMBAOMBA WAONDOLEWE KAMA ALIVYOFANYA MZEE MAKAMA ENZI ZAKE ZA UKUU WA MKOA WA DSM. BIG TO YOU PMAKONDA. KEEP IT UP.

  ReplyDelete
  Replies
  1. 🍸this is for you u said it all
   Makonda is a very hardworking leader we hope for the best πŸ™

   Delete
 2. 50 kwa 50 bado kabisaaaa!!!

  ReplyDelete
  Replies
  1. Endelea kusubiri hapo hapoπŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰πŸ˜‰

   Delete