asas

asas

sintah

sintah

RAIS MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI ENG WILLIAM KIJAZI

Ikulu Dsm
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​ 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Hafla ya kuapishwa Balozi Kijazi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu na Naibu Katibu Wakuu. 

Balozi Kijazi ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India, anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine. 

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na Mwakilishi wa Shirika Ia Umoja wa Mataifa Ia kuhudumia wakimbizi hapa nchini (UNHCR) anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amemshukuru kwa kazi kubwa ya kuhudumia wakimbizi kwa kipindi chote alichokuwepo hapa nchini. 

Kwa upande wake Bi. Joyce Mends-Cole amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Tanzania kuzisaidia nchi zenye matatizo, hususani migogoro ya kisiasa ambayo husababisha watu wake kuwa wakimbizi. 

Pia amepongeza kuteuliwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kusaidia usuluhishi wa mgogoro wa Burundi ambao umesababisha idadi kubwa ya wakimbizi kukimbilia Tanzania.

Hata hivyo amesema idadi ya wa kimbizi wanao kimbilia Tanzania imepungua kutoka wakimbizi 3,000 waliokuwa wakiingia hapa nchini kwa wiki, wakati Mgogoro wa Burundi ulipoanza hadi kufikia wakimbizi takribani 1,000 wanaingia hapa nchini kwa wiki hivi sasa. 

Aidha, Bi. Joyce Mends-Cole amewashukuru watanzania kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi cha miaka mitatu aliyofanya kazi hapa nchini, na ameahidi kuwa Balozi wa kuitangaza vyema Tanzania. 
 
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es-salaam

4 comments:

 1. Hebu leta story za kuchangamsha kichwa tupate mudi ya kazi sinta. hii habari hainibambi hata.

  ReplyDelete
 2. Wale mnaopenda kulalamika leta habari za muhimu mko wapi kucoment? mkiletewa habari za maana mmekimbia, ukiletwa umbea sintah tuandikie ya maana mko wapi mbona hamkomenti? kinachotuleta humu ni umbea mkome kumsema Sintah akileta umbea

  ReplyDelete
 3. Yani watz vilaza ni shida hbr ya muhimu coment 2 zikiletwa za umbea sintah mnafiki mnataka nini mbona ambebeki kama njiti wa kwa Obama lol

  ReplyDelete
  Replies
  1. kumbe shoga angu umeona eehhh!!! watz hatujielewi tupo tupo kama ngano kila aina ya style inatumiwa kwa ngano
   sintahh kuanzia leo weka habari unavyojisikia afterall hii blog ni yako sio yetu so wakuwacheeeeee mtt ya kipare
   wenyewe wamekimbilia kwa sintah kwao kumedoda wamebaki na IG tu chezea wewe
   nakupenda sintah mana huna show off za ajabu
   afu nimegundua kuna watu ni vilaza kweli wanataka sintah uwe kama njiti kitu ambacho hakiwezakani coz wewe na yy ni tofauti ndo ukaitwa sintah na yeye jina lake

   Delete