asas

asas

sintah

sintah

ZANZIBAR NI YA SHEIN

Rais Mteule wa Zanzibar Dr Shein
Hatimaye Zanzibar imepata wa kuiongoza kwa kipindi kingine cha miaka 5.... Dr Mohamed Shein alitangazwa kuwa mshindi jana kwa 91-4% hivyo kuipelekea CCM ushindi mnono.... hata hivyo umoja wanaounda Nchi za ulaya (EU) na marekani  kupitia mabalozi wao hapa nchini Tanzania wameukosoa uchaguzi wa marudio na kusema haya:

Tumesikitishwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wa kuendesha marudio ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, bila kuwepo makubaliano ya pamoja baina ya pande kinzani na ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani humo uliotokana na majadilino baina ya pande husika. 
 
“Ili uwe wa kuaminika na kukubalika ni lazima mchakato wa uchaguzi uwe jumuishi na unaowakilisha kwa dhati matakwa ya watu.
 
“Tunarejea wito wetu kwa Serikali ya Tanzania kuonyesha na kuchukua uongozi katika suala la Zanzibar na kujielekeza katika kupatikana kwa ufumbuzi wa mgogoro huu kwa kupitia mazungumzo baina ya pande husika kwa lengo la kudumisha amani na umoja katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
“Kwa mara nyingine tunawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa utulivu na ustahimilivu waliouonyesha katika kipindi chote cha mchakato huu na kuvitaka vyama vyote na wafuasi wao kuanzisha tena mchakato wa maridhiano ya kitaifa ili kupata ufumbuzi jumuishi, endelevu na wa amani.”

No comments:

Post a Comment