asas

asas

sintah

sintah

RAIS MAGUFULI AMFUKUZA KAZI ANNA KILANGO MALECELA

aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  mama Anna kilango Malecela kuanzia leo.

Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati, Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa  sana na hali hiyo.

Amesema idadi ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili za mkoa huo bado zinaendelea kuhakikiwa.

Rais pia ametengua uteuzi wa  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.
 
Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi akiwa amedumu katika nafasi hiyo kwa mwezi mmoja tu..
 

7 comments:

 1. ehhheeee endelea baba magufuli, wapangue tuu hawa wamama wa mujini...nchi umeendeshwa kiholela ilimradi wewe hawara wa kibopa...# poleni glam madam nafue, nacky na ikumbo! pozi kufa

  ReplyDelete
 2. Duh!Twamkaribisha uraiani sijui atatoa wapi pesa ya mukorogo. Huyu mbona anaonekana mkali sana khaa. Alitakiwa kuwa mwalimu mkuu wa primary na si mkuu wa mkoa. Ni mukali sana huyu wajameni(in haya voice).

  ReplyDelete
 3. Mtasubiri sana mwenzenu kaambiwa atapangiwa kazi dua la kuku alimpati mwewe mwenzenu ana elimu Na ni mpiganaji awo watoto wake wapiganaji nyie endeleeni kushinda mitandaoni

  ReplyDelete
  Replies
  1. Wapiganaji??wanaitwa bondia nani na nani? Sijawahi kuwasikia hawa!

   Delete
 4. Hakuna kujuta kabisa muacheni mama mkwe wangu 👍 anapesa za kufa mtu

  ReplyDelete
 5. Awatoe tu wengi wanafanya kazi kwa kubebwa kwanza wameshazeeka watoke tu vijana kibao hawana kazi

  ReplyDelete
 6. MKUU TUNAKUOMBA MPANGIE KAZI NYINGINE HUYU MAMA PLEASE, NI JEMBE.

  ReplyDelete