sintah

sintah

aka

aka

OUT OF TOPIC DAY

Dear Sintah.com Readers, 


Leo ni siku nyingine tena ya OOTD kama umeguswa na kitu, mtu kakuchefua, mtu unampenda sema unashindwa kumwambia na mambo mengine katika jamii ambayo tunapaswa kutafahamu , story za hapa na pale tukisogeza huu mwezi wa ramadhani....

ila leo katika OOTD  naomba niulize swali ikitokea marafiki wawili ku share bf halafu baadaye wakarudiana na kuwa ma bff hivi unakuwa ni urafiki wa ukweli ama wa kichina???

WENYE HELA WANAFAIDIII JAMANII

muke ya Jay Z

mali ya kaka kubwa hapana chezeyaa

CHEKECHA, CHEKETUA YES OR NAHWataalam wangu wa kudadavua mambo je hii Video ni YES  or NAH??? By the way unafikiria hii video  imefanyiwa wapi?

drop ya comment

THE DEVIL IS AT WORK

 so called  diva

Mungu babaaaa ulegiiii

Bruce Jener go back inside n dress

whyyyyyy??? uso umemkomaa kabisa

heels on
kamuiga ex wife mambo ya animal print dress


Heeeeeeeee bandugu mambo yamefika huku aisee, nilijua utani kumbe  serious huyu baba hasa anataka nini? ni attention ama? na mwendo kabadilisha kabisa na mini skirt anapiga eeeh Mungu baba hizi ni nyakati za mwisho kwakweli....

TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA

 Our lovely viewers 

leo tulikuwa tunarekebisha mitambo yetu hivyo tulikuwa hatuko hewani kwa muda wa masaa fulani hivi yote ilikuwa ni kuweka sawa mambo na nashukuru kila kitu kimeenda sawa

tumerudi hewani kwa wale ambao bado mnasua sua kutupata refresh na utatupata kama mwanzo..

tell a friend n tell a friend 

tunawapenda sana.....

Sintah.com

WASANII NA SIASA 2015

Irene Uwoya
Wema Sepetu
Steven Mengele

Dear dada Sintah......

leo naomba wanajamii tuwe tofauti kabisa, tumekuwa tukisikia na kuona baadhi ya wasanii wakitangaza nia ya kugombea nafasi tofauti katika taifa letu' je ni kweli wanaelewa changamoto zinazokabili  taifa hili?wanasifa, uwezo, heshima na nidhamu ya kuwa viongozi? je kila aliyemaarufu anafaa kuwa kiongozi? au wamekurupuka? mkumbo kwasababu fulani katangaza na mie nifanye?au soko la sanaa limekufa?ama sanaa imewashinda?

hapo juu ni baadhi tu ya wasanii waliotangaza nia ila wasanii wapo wengi na si wa movie tu na waimba bongo flava.

tujadili...

I do the seeking n you do the judging.......

WIFI WA TAIFA YAMEMFIKA HAPA!!!!
wifi wa Taifa, akijibana namna hii mnasema ooh anambana mtoto akijiachia na magauni yake ya free hapendezi kweli wanaadam whawana jema, muacheni mtoto wa watu si mara ya kwanza kubeba mimba anajua anachofanya......
Hahaaaaa unaweza ukawa mvumilivu na ukashindwa aisee, watu na maneno mengi aiseee uwiiii nafwa, kawapasha wale vizabi zabina wakapashika na mkome tena kuwafuatilia watu mambo yao anavaa viatu virefu mimba kakubebea wewe....au ndio mnajifanya mnajua watu kuliko wenyewe wanavyojijua ...... kawapa za uso vizabi,

wajameni hata hivyo kwa wale mliowahi kubeba mimba hivi mmegundua ukiwa mjamzito kuna Doctors  and Nurses wengi huko kitaaani kila mtu anasema lake as if uliwaomba msaada, ama wewe huendi kwenye antenatal clinic  kusikiliza Dr anasemaje wao ndio wajuaji huko mtaani, mimba kabeba yeye kuumia unaumia wewe mbona majanga mbona mabigggggg

kwaheriiii.......

NYWELE , NYWELE, NYWELE

hapa kuna wigs, weaving etc sporah hairNywele Original ziliopitiliza, ni kutoka kiwandani kabisaa, ni  kwa Sporah tuuu, kwengine kote zuga, hebu ona nywele zenye ubora wa hali ya juu.....kwa mahitaji yako ya nywele za ukweeee nenda www.sintah.com pia wanafanya online service hebu kuwa mmoja kati ya wale wanaoamini nywele ni Sporah tuuu wajameni ngoja Ramadan iishe niweke yangu ya ukweee, pia wana wigs usiogope bei maana maisha ni mafupi mno watu siku hizi wanachukua no kama hawana akili nzuri tumia pesa ikuzoeee... thou inaweza ikawa bei ya kodi ya mwaka mzima maana ni 2m na above .........

BUNGENI BUNGENI 2015 NI BALAAAA

Irene Uwoya
Wanawake wakiwezeshwa wanawezaaaaaaa, haya mdada mwingine kutoka Bongo Movie anayetaka kwenda kwenye siasa Irene Uwoya, yupo gado kuingia katika kinyanganyiro cha ubunge kupitia CCM, uwiii CCM ya mwaka huu ni balaaa, wa Tanzania mpo tayari kumpokea mwana kutoka Bongo Movie kama Mbunge???


BIASHARA NI MATANGAZO- WOLPER AJIGAMBA YEYE NI FREEMASON


Kuna vitu na vitu vya kukaa mbele za watu na kuwa navyo proud wapendwa ila sielewi my dear Jackie kujisifu kama yeye ni Freemason ni  jambo muhimu ama waliomhoji wameongeza chumvi zao, kama amesema kanisikitisha....

DR ASHA ROSE MTENGETI MIGIRO ATUA NYUMBANI

Dr Rose akiwa na list yake ya wadhamini Mwanga Kilimanjaro
Dr Rose Migiro akipokea majina ya wadhamin toka kwa katibu wa CCM Mwanga Bi Mwanaidi
Dr Rose akiwa na kaka zake kwenye kaburi la baba yake Cheif Shaaban Mndorwe Mtengeti Sangiwa II na babu zake waliotangulia.

OUT OF TOPIC DAY (THURSDAY SPECIAL)

Ni siku nyingine tena ya kupashana habari za hapa na pale, yaliyojiri  kwenye maisha  yetu ya kila siku, nani kapata zali nani anahitaji mchumba, nani kaachwa lolest , nani week imemuendea vibaya, nani  anahitaji umshauri? haya karibuni jamvini.......

SHAKE MY HEAD......LOLESTHakiii hii Dunia haina mambo ila wanaaadam wana mambo sana wajameni, sikuwahi fikiria kama kuna mtu atatoa boko kama hili aiseeee,.

I do the seeking and you do the judging ........

LINA AOPOA KITU KIPYA

ma love loveeeeKatika vitu ambavyo naomba Mungu anisaidie nikuhama  huu mji maana mambo ni mazitooo, mji huu wa drama,mikimikii, ku fit in una raha yake kila siku kukicha sie bloggers hatulali njaa, maana vituko vya mastaa vinatufanya tunanunua nywele za sporah haaaaaa Lina ameopoa boss mutotoooo na dada yetu naye ataenda kule kwa basebo na banyabo akapike matoke, waganda mmeamua kwa mambo haya kweli umoja wa Nchi za Afrika Mashariki udumuuuuu.....

Jamaniiii Waganda imetoshaaaaa khaaaa mmetuamulia??

SUGU YAMEMFIKA YAKUMFIKA, SASA AENDA MAHAKAMANI

daaah maskini huyu mtoto baadaye anakuja kuonyeshwa pics za mama yake, anaweza akapiga ukungaaa, na hivi ka kike, poor her
mwanamke mjinga ataivunja ndoa yake yeye mwenyewe kwa mikono yake tena miwili, huyu kavunja na mikono sita


Mbunge wa Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’ amemfikisha kortini aliyekuwa mkewe,  Faiza Ally akitaka apewe mtoto wao, Shaa (2) ili amlee kwa vile mama yake huyo si mwadilifu.

Ijumaa iliyopita, saa 2:00 asubuhi, Faiza alipanda kwenye kizimba cha Mahakama ya Mwanzo, Manzese/ Sinza iliyopo Sinza-Makaburini jijini Dar kwa ajili ya kukabiliana na madai hayo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mheshimiwa Sugu alifikia hatua hiyo baada ya kuchukizwa na tabia mbaya za mwanamke huyo hasa ya kuvaa nguo zinazomuacha nusu utupu na kupiga picha za aibu, akiamini kuwa, tabia hizo zinaweza kuathiri makuzi ya mtoto huyo.
 
Chanzo  hicho kiliendelea kusema kuwa, kwa kipindi kirefu, Sugu amekuwa akimvumilia Faiza, lakini hivi karibuni uzalendo ulimshinda baada ya picha zake akiwa amevaa kigauni kifupi na makalio nje kusambaa mitandaoni.


Akizungumza mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Patrick Vaginga, Mheshimiwa Sugu alidai kuwa mbali na mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kuvaa nusu utupu pia ana mtindo wa kupiga picha zisizo na maadili na kuziweka mtandaoni yeye mwenyewe.

Sugu alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, pia mwanamke huyo amekuwa na tabia ya kumpiga picha mbaya mtoto wao na kuzimimina humohumo mitandaoni jambo ambalo alisema linamharibu mtoto huyo.

Mbali na sababu hizo, pia Sugu aliongeza kuwa, Faiza hana kipato kizuri cha kuweza kumlea mtoto na mara kwa mara amekuwa akisafiri jambo ambalo husababisha mtoto huyo kutopata malezi ya mama kwa muda mrefu hivyo kuiomba mahakama impe haki yeye ya kuishi na mwanaye.

Naye Faiza akijibu mapigo katika utetezi wake alisema kuwa, Sugu hafai kumlea mtoto huyo kwa sababu naye ana tabia ya kusafiri kwa muda mrefu hivyo kuishi mbali na mtoto ambapo aliiomba mahakama hiyo isimruhusu baba mzazi huyo kuishi na mtoto kwa kuwa atamharibu.
NB
hatimaye kelele zetu zimesaidia bandugu na hatimaye Mh Joseph afungua kesi, mmmh mabig lengo la hii website ni kurekebisha tabia/ kuburudika na si kuwa na chuki na mtu na sie hatujibizani na mtu sie tunandika kama wadau na ni jukumu letu kuielezea uma, weye ukijibu huko tunafurahi coz unatuongezea viewers.....

ila ndugu zangu hivi ni mimi tu ama,  simuelewi Faiza unajua kuna mambo anayoyafanya mpaka yananishangaza hivi unaendaje kuwa interviewed na ukasema tumekutana fb?? really wenzio huwa wanaficha lakini wewe ndio unajianika jamani twendeni mbele na kurudi nyuma a lil bit of education helps hivi hana wazazi ama washauri? ama ndio wale watoto watukutu mpaka mama anapata headache ...... acheni niendelee kuteseka shuleni wajameni ndio maana najua kuchuja pumba na mashudu.....

OUT OF TOPIC DAY

Kama kawa ni jumatatu nyingine tumshukuru Mungu kwanza kwa pumzi, pili mwanawane weekend ilikuwaje? kuna mambo gani yalitokea hapo kitaani, mwezi wa ramadhani umekatisha mambo ama watu bado wanakula bata, mambo gani basi unayaona ya muhimu ambayo yametokea weekend na leo Monday tuyajadili?? huu ndio uwanja wako maalumu wa kujadili mambo yoteee ya kijamii na hususani yale tusiyoyajua tunayafahamu hapa maana wanajamii mbalimbali yanakuwa yamewakuta kwa namna moja ama nyingine

karibu sana katika OOTD...

Please maneno ya ajabuuu kuntu mwezi huu uheshimiwe....

UNAWAFAHAMU WANAWAKE HAWA???

Asha Rose Migiro

Monica Mbega

Mwele Malecela
Amina Salum Ally

Kila siku katika blogs/magazeti tunaona wagombea waliojitokeza kugombea Uraisi katika CCM ni wanaume tuuuu, wakina mama vipi sasa basi kwa leo nawaleta kwenu wakina mama waliothubutu kuchukua form za kugombea Uraisi endapo chama chao kitawaruhusu kutana na majembe haya manne... kama ulikuwa huwajui sasa wafahamu....wanawake tunaweza

UNENE HAUNA DEAL KABISAAAA

Meek Mill n Rick Ross


Muone muimbaji Rick Ross aliekuwa jitu la miraba minne na sasa yupo kama Meek Mill, mwanawane kazana  kuondoa hayo mafuta....

TUNAANZA WEEKEND NAMNA HII

huyu ndiye aliyemuwanza mwenzie kwakweli, mashabiki nao wanakata stimu
haaaaa Mondi akampa kidochi, akalalie mbele


Diamond limemfika hapaaaaaa, in Soud Brown's voice nimecheka mpaka naumwa ila kweli sie tulioweka family yetu mbali nao wanatusema, wale wanaoonyesha wanasemwa heeee binaadam mnataka lipi haswa???


Diamond yamemfika hapaaaa?? jipostie unachojisikia Mondi ni acc yako na kwa raha zako asiyetaka ana uhuru wa kubonyeza kile kidude cha kijani kuwa blue. free world mweee

FUTURE AFUMANIWA TENA

Future ana mambo

Yaani usijidanganye eti mtu ukimfumania mara moja ataacha hio tabia aaaah wapi bandugu yaani ndio atazidisha hatari once a cheater always a cheater... baada ya kumwagana na Ciara, Future akarudi kwa baby mama wake mwingine maana huyu naye kazidi kwa ma baby mama kavunja record sasa hivi majuzi baby mama huyo Brittni Mealy amemfumania tena daaah huyu Future ni balaaaaaaa

mwanamke acha kuwa na akili ndogo ukimuona baby wako ana baby mama tayari usiwe na akili iliyo ndani ya uvungu na wewe ukaenda kubeba mimba ukawa baby mom wa pili perhaps watatu, hebu jaribu kuwa tofauti kidogo fanya kazi ya ziada ili wewe uolewe uwe tofauti nao, nakupa rules hizo u will thank me later 

SINA MAJINA YA MAFISADI INGAWA UOVU HUU UPO NDANI YA VYAMA VYA SIASA

Mh Wassira
MGOMBEA anayeomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Steven Wasira, amesema hana majina ya washukiwa wa ufisadi, ingawa uovu huo umo ndani ya vyama vya siasa ikiwamo CCM.

Wasira anayeongozwa na kauli mbiu ya Uadilifu na Umoja wa Watanzania; Safari ya Uhakika, alisema hayo wakati akizungumza na wana-CCM waliomdhamini katika mikoa ya Rukwa na Katavi jana.

Alisema CCM na serikali yake ni taasisi zilizo na misingi ya uadilifu, ingawa ndani yake kuna uwezekano wa kuwapo watu wanaotuhumiwa kwa uhalifu huo.
Alisema ufisadi na rushwa na miongoni mwa matatizo makubwa yanayoiathiri jamii na kwamba taifa linamhitaji kiongozi asiyekuwa na kashfa inayomfanya atiliwe shaka katika kukabiliana na kadhia hiyo.

“Hapa sina majina ya mafisadi lakini ninaamini kwamba si ndani ya CCM pekee, bali hata katika vyama vingine vya siasa, rushwa na ufisadi ni miongoni ma matatizo makubwa yanayovikabili,” alisema.

Wasira alisema kutokana na hali hiyo, vita dhidi ya rushwa na ufisadi inapaswa kuwa katika misingi ya hoja na uthubutu wa kuidhibiti badala ya kumlenga mtu binafsi.

Alisema Tanzania ina taasisi imara ambazo zikitumika ipasavyo zitachochea kuwatambua washukiwa wa ufisadi,  vitendo vinavyoashiria uhalifu huo na kuchukua hatua kwa ukali na haraka.

Wasira alisema ikiwa CCM itamteua kuwania na hatimaye kuwania Urais, imani yake ni katika kutoa uhuru na mamlaka zaidi kwa vyombo husika vikiwamo vya sheria, kutekeleza majukumu bila kuoneana aibu.

Alisema, “ninapozungumzia ufisadi sizungumzii mtu au watu, tunauzungumza ufisadi kama hoja, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba hata ndani ya CCM kuna viashiria vya ufisadi, lakini haimaanishi kwamba CCM ni chama cha kifisadi.”
Aliongeza, “hata kwa upinzani kuna ufisadi pia, hivyo ufisadi ni tatizo kubwa katika jamii yetu, kama nitapata fursa ya kuliongoza Taifa letu nitahakikisha tunaukabili kwa nguvu zote ili kurejesha heshima na hadhi ya nchi yetu,” alisema.

Alisisitiza umuhimu wa kupiga hatua katika kilimo na viwanda ikiwa ni moja ya njia kuu za kukuza uchumi na kuboresha maisha na ustawi wa wananchi.

Kwa mujibu wa Wasira, kilimo pekee ndicho kinaweza kuzalisha ajira nyingi kwa vijana kuliko sekta nyingine pamoja na kuliingizia Taifa pato kubwa zikiwamo fedha za kigeni.

Wasira alizungumzia ajira kwa vijana na kusema hivi sasa kuna kasi ya vijana wengi kukimbia kutoka vijijini kutokana na umasikini unaowakabili, na kwenda kukutana na umasikini mwingine mijini.

Alisema uboreshaji wa kilimo, uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vya kuongeza thamani za mazao kutatoa hamasa kwa vijana kushiriki kilimo na kutengeneza ajira.

Leo Wasira anatarajiwa kuwasili mkoani Kigoma kutafuta wadhamini, ukiwa ni mkoa wa 30 tangu aanze safari ya kutafuta wadhamini Juni 3, mwaka huu ambapo alianzia mkoani Dodoma.

Vikao vya uteuzi vinatarajiwa kuanza mjini Dodoma Julai 5, mwaka huu, ambapo mgombea urais kwa tiketi anatarajiwa kupatikana Julai 11, na Uchaguzi Mkuu umepangwa kufanyika mwezi Oktoba.

Mwisho

MAAJABU YA KARNEVijana wamethubutu hivyo muwape nafasi maana tunataka kuondoa wazee bungeni waingie wao vijana ili waweze  kutetea taifa hili mfano Prof Jay, Afande Sele na wengineo, hivyo basi support Wema Sepetu na Singida yake, usiwe na roho ya kwanini ama fulani hawezi hata huyo Amina mnaemsema mlishawahi kusema hawezi na akaweza na wangapi wapo Bungeni wadada kama yeye? kwanini wao waweze na yeye asiweze?

ila Bungeni kutakuwa na shughuliiiii daaah aiseee ni balaaa
 .....
GO, GO WEMA SEPETU

VOTE VOTE MONDI BIN LADEN NA VEE MONEYKwa mara nyingine tena wa Tz wanaweza kuingia ktk kinyan'ganyiro cha tuzo na kwa sasa ni tuzo za MTV kinachotakiwa ni vote yako ili tuweze kutoboa usidanganyike kwani umoja ni nguvu utengano ni udhaifu sasa basi wapigie kura kila dakika ili tuweze kuwashinda wa Nigeria, unajua wa Nigeria wamekuwa nominated wengi ktk hivi vipegele inamaana kura watagawana si eti eeeeeh basi wakigawana sie tunapeta,,, VOTE VEE MONEY NA DIAMOND  fastaaaaaaaa ...... acha ushabiki maandazi usio na faida

BASI LA TAIFA STARS LAPIGWA MAWE
Kufanya vibaya katika mashindano mbalimbali ya Africa, wa Tanzania wamechoshwa kila siku kuwa mkia, na mpaka viongozi mbalimbali wamekatishwa tamaa, sasa wananchi wameamua kulipiga mawe gari la Taifa Starzs sijui Jamal Malinzi afanyaje Mungu wangu maana anatakiwa kutuliza kichwa chake haswa na wakati mwingine wala si wa kuwalaumu ni wachezaji wenyewe maana  mtu anaejua ana match anaenda club na usingizi juu na demu anapata unategemea atafanya vizuri?? wachezaji nao wanajisahau sana .........

UNA NDIMU, LIMAO, AMA VINEGAR???

siku hizi ukiwa na baby lazima ajiweze
Habariiiii ya mujini, town na vitongoji vyake, siku hizi ukiwa na baby lazima awe na ankara sio  kila siku kupiga mizinga tuuu oooh baby naomba hela ya salon mara vile natakiwa kwenda ngomani inahuuuuuu? siku hizi wanaume wanajua pakujiweka shosti weeee si kwa matonya style hebu niishie hapo ...... je wewe mwenzangu unachagua nini kati ya ndimu, limaoama vinegar shosti mie nimechagua ndimu.....

MAUZAUZA YA MWAKA

ni balaaaa

hii ni sifa ama? hebu tumkalie kitako huyu binti kwa siku ya leo

wakati mwingine lazima ujiulize hivi sie binaadam zimo kichwani ama, mtoto mwenye heshima aliyezaliwa na wazazi wake no matter what hawezi kufanya huu ujinga, huyu ndio maana sugu alimpiga chini maana aliona mbali, mtu anawakilisha jimbo anakuwa na demu mcharuko zaidi ya dagaaa katika  chungu? uvaaaji gani huu yarabi but somehow i blame kwa waliotoa kadi maana utapelekaje watu kama hawa katika awards? mnaacha kuwapa watu wa maana na shughuli zao mnawapa watu wanaokuja kutega mingo, maana kama sio kutega mingo hiki ni nini?? anyway Mh Sugu kaa na mzazi mwenzio umwambie maana tangu aachane na wewe naona zimemruka kichwani , hata kama hupo naye ila ana mtoto wako unakubalije mama wa mtoto wako akafanya haya maajabu ya kishetani  bora ajiuze kimya kimya kuliko kama hivi watu wanasema demu wa Sugu mptuuuu kwakweli Faiza unatia aibu  unajaribu so hard lakini wapi?? tatizoooo nyota ipo siku utakunya stand wewe kwa mwenendo huu wa kutaka umaarufu kiulazima

kwani hujawahi kuona watu wakienda sehemu kama zile wanatakiwa wavae nini?? halafu siku hizi wanaume wamejanjaruka hawataki cheap products kajipange upya
ila marafiki wabayaaa na ma snitch sasa mnamuachaje anatoka hivi ama ndio hasikii kupitiliza yaaani mie ndiye ningekuwa but haiwezi kutokea nikawa rafiki yake ningemchapa kwanza its so disgusting, nasty ptuuuuuuu

SPORAH AZINDUA BIDHAA ZAKE

super

kwa wapenda ma wig ni balaaa yaani original iliyopitilizaaa


Hahaaaa Bidhaa za dada Sporah zipo tayari ma Diva wa ukweli mkae tayari maana msidanganyike na nywele zisizokuwa na afya katika vi cosmetic shop mchwara kila mtu anajifanya anauza nywele za uhakika siku mbili siku, nywele zinageuka kuwa fagio , mambo yapo  Sporah bwana ni gharama lakini ni nzuri na ya kukaa muda sana

Nilikuwa nazisubiria kwa hamu hatimayeeee ngoja nianze na mie ili niwape mfano

Dada Sporah najua u my no one fan , usikopeshe haaaa batoto ya Dar ni noumaaa wakija waje na cash

WEEKEND NJEMA

mom to be,jamani wale ndugu zetu wajawazito mnafanya mazoezi?? igeni mfano huu

ila Zari mimba immempenda
baba na mama Kijacho

Mahaba niteketezeeee, mahaba niuweeee mahaba nijiachieee hivi kwa sisi wanawake kuna raha mtu anapenda kama pale ni mjamzito na baby yupo pale 24/7 yaani unatamani hata usijifungue na hata kama sio mjamzito mie ninaona mapenzi ni kumjali mtu bana sio pesa ndio maana mtoto mlito Zari katulia kwa kaka dimondo....

hivi unakubaliana na mimi kuwa hii ndio powerful couple East and Central Africa? utafiti umefanywa na kugundua hili kwamba kwa sasa hawa ndio wanaumiza watu katika social media kama ulikuwa hujui ndio jua sasa