Monday, September 15, 2014

INSTAGRAM KUNA MAMBO

tusio na waume tunakomaaa
Yesu baba rudiiii, khaaa wakati wiengine wanatumia fursa za mitandao ya jamii na kujipatia fedha,wengine wanatumia kulumbana... hii inaitwa akili ni nywele kila mtu ana zake....

Monday, September 15, 2014

MAJUTO NI MJUKUU

baada ya kufanya maloloso

hiki ndicho alichoandika mmiliki wa mgahawa

Wakati dunia nzima inapinga ubaguzi wa rangi, mwenzetu huyu kumbe yupo hapa kwetu ilimradii tu, maana unatutukana sie katika nchi yetu anyway wabongo wengi wamesisitiza kutoenda katika mgahawa wake kwa kile cha kwamba amedhalilisha watu.... jamani ukiwa na hasira usitumie social network maana unaweza ukaandika kitu cha ajabu kikakufanya ujutie sana kama huyu mama anavyojuta sasa hivi...

Saturday, September 13, 2014

WEEKEND LIFE STORY

nina mpenzi wangu ambaye toka tuanze urafiki tuna karibia mwaka wa tatu sasa,kipindi tunaanzana alikuwa hana kazi,kwa maana kwamba mimi nilimkuta akiwa hana kazi japo katika maelezo yake ni kwamba alikuwa na kazi lakini aliachishwa,na mie sikutaka kujua sababu,kipindi hicho tunaanzana mimi nilikua na kazi yangu nzuri hadi leo,wakati huo yeye alikuwa ni mtu wa kubangaiza hapa na pale,lakini maisha yalisonga,tulipendana kwa dhati kwa kweli,mapenzi anayajua,na anajua mwanamke anataka nini,kiufupi he cares,so loving and all that a woman would wish for from a man,that was him,
 
Siku zilikwenda miaka ikawa inasogea,akapata kazi mkoani,kila baada ya wiki 3 akawa anarudi Dar likizo kwa wiki 2,mapenzi yetu yaliendelea kama kawaida,tulikuwa twasiliana kila mara,hata usiku wa manane bila wasiwasi wowote japo kila mtu yupo mbali na mwenzake.Siku hazigandi akajapata kazi nzuri Dar,hapo ndio story yangu inapoanzia,tokea apate kazi dar,ametokea kujifanya yupo busy,mawasiliano si kama zamani,hanijali tena,wakati hana kazi nilimtunza kwa kila kitu,vizawadi vya hapa na pale,pesa ndo usiseme,alikua ananiingia kwa gia za kila aina,mara nikopeshe ntalipa halipi,kwa vile nampenda sikuona tabu kuendelea kusaidia mpenzi wangu,lakini jamani,tokea apate hiyo kazi,hata handkerchief hajaninunulia,kuna siku kaniomba hela nikamtolea uvivu,na kumsema kuhusu ubahili wake,hadi siku moja nikajidai nina shida,kanitolea visingizio kibao etii ooh kwa nini hujasema jana,na mengine kibao nikaishia kupewa kilaki kimoja,tokea hapo,yeye ni wa kujishaua mara hivi mara vile
 
,lakini cha maana sikioni,kumpenda nampenda kweli lakini hii tabia ya kunigeuza mie mtaji sasa nachoka,nahisi hakuwa na mapenzi ya kweli ila kipindi kile alitaka tu kunitumia kwa kuwa hakuwa na kazi,naombeni wadau mnisaidie,nifanyeje,kama kumwambia nilishamwambia,lakini naona kama vile ni makusudi,jamani hata tu siku moja kuninunulia japo apple aniletee ni shida?lakini akiwa na shida utaona tu mawasiliano yanazidi wajua tu ni mzinga ndo kitakachofuata,nifanyeje na tabia hii,japo rohoni nampenda sana

Friday, September 12, 2014

ANAOMBA MSAADA

 Mie ni mdada wa miaka 31 naishi Europe sina mume wala mtoto, nimekutana na mkaka(kwenye tamasha) ni mwanamuziki sio mtz, story ndefu kidogo ila tulianza kama marafiki sasa tuko kwenye mapenzi mazito japo hatujadoo bado ila tatizo ana mke na watoto wawili na kwa jinsi nionavyo na tatizo na mkewe na anampenda japo anasema anatupenda wote, najua ni uongo wa wanaume.

jamani hakuni mtu alikuwa anawalaani watembea na waume za watu kama mimi ila husiombe yakukute. nafsi inanisuta kwa muda wa miezi mitatu ya kujuana nishamwambia tuachne zaidi ya mara nne ila ndo kama mnavyowajua wakitaka nyapu wataongea maneno yote nami vile nampenda namkubalia. sasa anataka kuja kunitembelea in two weeks time na hii tuliplan zamani kidogo ila nafsi yangu haitaki, msaada ni kwamba naomba hii mniwekee kama mada na mnachambe bila huruma yaani mnipe maneno ya karaha hasa ili kila nikikumbuka yaniumize hata akisema vipi nisiwe nae. Sintah naomba uitoe hii...